Picha : MWENDESHA BAISKELI 'DALADALA' AUAWA KWA KUPIGWA GONGO MJINI SHINYANGA

Jeneza lililobeba mwili wa mwendesha baiskeli 'Daladala' aitwaye Daudi Jilala (24) 

Daudi Jilala enzi za uhai wake.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog 

Mwendesha baiskeli anayebeba abiria maarufu Daladala aitwaye Daudi Jilala (24) ameuawa kwa kupigwa kitu kizito kichwani na mtu/watu wasiojulikana chumbani kwake katika mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga. 

Mwili wa marehemu Jilala umebainika kuwa ndani ya chumba chake Jana Jumatano Januari 15,2020 majira ya saa tano asubuhi baada ya majirani zake kuhisi harufu kali na nzi kuonekana wakitoa chumbani. 

Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa Daudi Jilala alionekana kwa mara mwisho mtaani siku ya Jumapili Januari 13,2020 na hakuonekana tena hadi alipokutwa ameuawa ndani ya chumba chake kwa kupigwa na kipande kikubwa cha mti ‘gongo’ kichwani linalodaiwa kukutwa na damu ya marehemu. 

Inaelezwa kuwa siku hiyo ya Jumapili alionekana akiwa na kijana mgeni mtaani ambaye hajulikani alitokea wapi na hajulikani alipo na kwamba baiskeli,pesa na simu ya marehemu Daudi vimeibiwa.

Akizungumza na Malunde 1 blog, Jesca Simon ambaye ni jirani yake na marehemu amesema alikuwa anahisi harufu akadhani ni harufu ya choo kilichopo jirani na chumba cha marehemu na baadaye akafuatwa na majirani wanaoishi karibu na nyumba aliyopanga ambao walitaka kitu gani kinasababisha harufu kali eneo hilo ndipo wakabaini kuwa inatokea ndani ya chumba cha Jilala.

“Tulipoingia ndani tukaona mtu amelala kitandani tukaenda kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa ambaye alifika chumbani na kuwaita viongozi wa ngazi ya kata wakatoa taarifa kwa jeshi la polisi ambalo lilifika na kuuchukua mwili wa marehemu”,ameeleza Simon. 

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mabambasi Bakari Hamis ameiambia Malunde1 blog kuwa,alipewa taarifa kuhusu tukio hilo na jirani yake na marehemu aitwaye Jesca Simon ambaye aliamka asubuhi na kuona mlango wa marehemu ukiwa wazi na uwepo wa harufu pamoja nzi eneo hilo. 

“Nilipofika nilikuta mlango wa chumba anacholala marehemu ukiwa wazi,pazia linaning’ing’inia ndipo nikabaini kuwa harufu iliyopo eneo hilo ni ya mtu,nikawasiliana na viongozi wa ofisi ya Mtendaji ya kata,tukawasiliana na polisi ambao walifika hapa kufanya ukaguzi na Daktari akampima marehemu na kubaini kuwa kifo cha Daudi kimesababishwa na kupigwa kitu kizito”,ameeleza Hamis. 

Akizungumza wakati wa kuaga mwili wa marehemu Daudi Jilala ili kuusafirisha kwa ajili ya mazishi katika kijiji cha Ng’wabagalu kata ya Nyabubinza wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, mwenyekiti huyo wa mtaa amewataka wananchi wa mtaa wa Mabambasi kuyapenda maisha yao kwa kuzingatia usalama wao. 

“Naomba myapende maisha yenu kwa kuzingatia usalama wa maisha yenu,mnapopata wageni watambulisheni kwa majirani zenu na kwa viongozi wa serikali ya mtaa ili ajulikane anatoka wapi. 

“Unapopata mpangaji mtambulishe kwa uongozi wa mtaa,msipangishe watu msiowajua kwa ajili ya usalama wenu kwani wengine siyo watu wema. Tuna mpango wa kufanya utaratibu wa kuwatambua wakazi wa mtaa huu”,ameongeza Hamis. 

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Joseph Paul amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kuwa Jeshi la polisi linafanya uchunguzi na kuendelea kuwatafuta watuhumiwa wa tukio hilo. 

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mabambasi Bakari Hamis akizungumza wakati wa kuaga mwili wa marehemu Daudi Jilala leo Alhamis Januari 16,2020. Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda kijiji cha Ng’wabagalu wilayani Maswa mkoani Simiyu. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mabambasi Bakari Hamis akizungumza wakati wa kuaga mwili wa marehemu Daudi Jilala leo Alhamis Januari 16,2020.

Kiongozi wa dini akiombea mwili wa marehemu Daudi Jilala.

Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Mabambasi akitoa matangazo.

Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Mabambasi akitoa matangazo.

Mwili wa marehemu Daudi Jilala ukiingizwa kwenye gari kwa ajili ya kuusafirisha kwenda Maswa kwa ajili ya mazishi
Mwili wa marehemu Daudi Jilala ukiingizwa kwenye gari kwa ajili ya kuusafirisha kwenda Maswa kwa ajili ya mazishi.
Waendesha baiskeli 'Daladala' mjini Shinyanga wakijiandaa kumsindikiza marehemu Daudi Jilala aliyekuwa anafanya kazi ya kubeba abiria 'daladala' kwa kutumia baiskeli enzi za uhai wake ambaye amefariki dunia kwa kupigwa kitu kizito ndani ya chumba chake katika mtaa wa Mabambasi.

Gari lililobeba mwili wa marehemu Daudi Jilala likiondoka katika mtaa wa Mabambasi kuelekea Maswa mkoani Simiyu kwa ajili ya mazishi.

Waendesha baiskeli 'daladala' Mjini Shinyanga wakisindikiza mwili wa marehemu Daudi Jilala aliyekuwa anafanya kazi ya kubeba abiria 'daladala' kwa kutumia baiskeli enzi za uhai wake ambaye amefariki dunia kwa kupigwa kitu kizito ndani ya chumba chake katika mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.

Gari lililobeba mwili wa marehemu Daudi Jilala likiingia katika barabara kuu ya Shinyanga - Mwanza.
Waombolezaji wakiwa msibani wakati mwili wa marehemu Daudi Jilala ukisafirishwa kwenda Maswa kwa ajili ya mazishi.

Waombolezaji wakiondoka msibani baada ya mwili wa marehemu Daudi Jilala kusafirishwa kwenda Maswa kwa ajili ya mazishi.
Waendesha baiskeli 'daladala' wakiondoka msibani baada ya mwili wa marehemu Daudi Jilala kusafirishwa kwenda Maswa kwa ajili ya mazishi.
Waendesha baiskeli 'daladala' wakiondoka msibani baada ya mwili wa marehemu Daudi Jilala kusafirishwa kwenda Maswa kwa ajili ya mazishi.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527