JESHI LA MAREKANI LATUMA BARUA YA KUONDOKA IRAQ .....WIZARA YA ULINZI YAIKANA BARUA HIYO


Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Mark Esper amekanusha kwamba Ikulu ya Marekani ilikuwa inajiandaa kuyaondoa majeshi yake Iraq. 


Tangazo hilo limetolewa baada ya jenerali mwandamizi wa Marekani kumpa jenerali mwenzake wa Iraq barua inayosema kuwa vikosi vya Marekani vitaondoka Iraq katika siku na wiki zijazo. 

Mkuu wa kikosi cha Marekani nchini Iraq, Brigedia Jenerali William Seely alituma barua kwa kamandi ya operesheni ya pamoja nchini Iraq, nakala ambayo ilionekana na vyombo vya habari kadhaa ikiwemo shirika la habari la Ufaransa, AFP na Reuters. 

Barua hiyo ilisema kuwa vikosi vya muungano vinavyoongozwa na Marekani kupambana na kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS vitachukua hatua kuhakikisha harakati za kuondoka Iraq zinafanyika salama na kwa ufanisi. 

Lakini wizara ya ulinzi ya Marekani imekanusha kuwa inakusudia kuviondoa vikosi vyake Iraq. Esper amesema hakuna uamuzi wowote wa kuondoka Iraq.


Mkanganyiko huu umekuja mara baada ya jeshi la Marekani kumuua kamanda wa jeshi wa Iran Qasem Soleimani.

Jenerali Soleimani aliuawa katika mapambano ya anga huko Baghdad siku ya ijumaa baada ya rais Trump kuamuru wafanye hivyo.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527