JAFO AKABIDHI MASHINE 7227 ZA KUKUSANYIA MAPATO YA KIELEKTRONIKI

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa[TAMISEMI] Mhe.Seleman Jafo amekabidhi  mashine elfu saba ,mia mbili  na ishirini na saba[7227]  za kukusanyia mapato  ya kielektroniki [PoS]  kwa  serikali za mitaa huku akitoa kiama kwa halmashauri ambazo zitafanya uzembe katika ukusanyaji wa  mapato hayo.

Akizungumza jana  Januari ,22,2020  jijini Dodoma mbele ya wakurugenzi wa halmashauri,makatibu tawala wa  mikoa    ,Waziri Jafo amesema mashine hizo itakuwa ukombozi mkubwa wa ukusanyaji mapato na kuagiza Wakurugenzi kukusanya mapato vyema na haitakuwa kisingizio tena juu ya ukusanyaji mapato hayo.

Aidha,Waziri Jafo amesema pamekuwepo na suala la Wakusanya mapato  Wasiokuwa waaminifu kwa  baadhi ya halmashauri hivyo uwepo wa Mashine hizo itaongeza chachu ya Uwazi wa ukusanyaji mapato huku akiishukuru Wizara ya Fedha na Mipango kwa kusaidia Mashine hizo za PoS kwa kushirikiana na Serikali ya Norway.

Katika hatua nyingine Waziri Jafo ametoa rai kwa halmashauri ambazo  hazijalipa madeni ya Madiwani  kulipa mara moja kwani hadi sasa halmashauri kubwa inadaiwa  Milioni 758.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527