HALMASHAURI YA WILAYA YA USHETU YAPITISHA BAJETI YA SHILINGI BILIONI 30.7 KWA MWAKA WA FEDHA 2020/21

NA SALVATORY NTANDU

Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Ushetu mkoani Shinyanga imepitisha Makadirio ya bajeti ya shilingi bilioni 30.744  itakayotumika katika mwaka wa fedha 2020/2021 ikiwa na ongezeko la asilimia 16 ya bajeti ghafi ya mwaka 2019/2020.

Akisoma Bajeti  hiyo Jana Januari 21 mwaka huu  kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Ushetu, Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo Adrew Hagamu katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika makao makuu ya Halmashauri hiyo Nyamilangano.

Hagamu alifafanua kuwa  fedha hizo zimegawanywa katika makundi ya fuatayo, shilingi bilioni 2,522,160,000 ni fedha za makusanyo ya ndani, shilingi bilioni 19,551,691,536 bajeti ya mishahara - Ruzuku (PE), shilingi bilioni 2,159,872,650 bajeti ya Matumizi mengineyo, na shilingi bilioni 6,510,851,707 za program za maendeleo.

“Jumla kuu ya fedha ambazo tunatarajia  kuzitumia katika bajeti ya mwaka 2020/21 ni shilingi bilioni 30,744,575,893 , zitatumika kuendesha shughuli zote za umma ikiwemo kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo imepitishwa baada ya kuibuliwa na wananchi kupitia kamati zao za maendeleo alisema Hagamu.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,  Wandere Lwakatare alisema bajeti hiyo imezingatia vipaumbele vyote muhimu vya maendendeleo hususani katika sekta za afya, elimu, na Miundombinu  ili kuhakikisha kero zilizopo katika sekta hizo zinapatiwa ufumbuzi.

“Waheshimiwa madiwani tutahakikisha miradi  yote ambayo meiibua na imepitishwa katika  bajeti hii ya mwaka huu tunaitekeleza katika kata zenu,hakikisheni mnatoa ushirikiano kwa serikali katika ukusanyaji wa mapato husasani kati vyanzo ambavyo vipo katika maeneo yenu ya kazi” alisema Lwakatare.

Akizungumza kwa niaba ya Madiwani wa Halmashauri ya Ushetu Makamo mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Tabu Katoto ambaye ni Diwani kata ya Igunda alisema kuwa bajeti hiyo imezingatia mapendekezo ya miradi mbalimbali iliyoibuliwa na wananchi kupitia kamati zao za maendeleo za vijiji na kata.

“Nitoe rai kwa mkurugenzi na wataalamu wa halmashauri hii hakikisheni mnatekeleza bajeti hii kikamilifu ili wananchi tunaowatumikia wawezekufaika nay ale ambayo tumeyaahidi kuyatekeleza kupitia ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) fedha za miradi kama vile afya na elimu zipelekwe kwa wakatika katika maeneo husika”alisema Katoto.

Bajeti hii imeongeza kwa asilimia 16 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2019-2020 ambayo ilikuwa shilingi bilioni 25,892,445,461.

Mwisho.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post