IRAN YASEMA MASHAMBULIZI YA LEO DHIDI YA MAREKANI NI KAMA MAKOFI YA USO TU | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, January 8, 2020

IRAN YASEMA MASHAMBULIZI YA LEO DHIDI YA MAREKANI NI KAMA MAKOFI YA USO TU

  Malunde       Wednesday, January 8, 2020

Kiongozi mkuu wa  Iran, Ayatollah Ali Khamenei amesema hii leo kwamba shambulizi la makombora kwenye kambi za kijeshi zinazotumiwa na Marekani nchini Iraq ni kofi la uso kwa taifa hilo na  amesisitiza hatua hiyo ya kijeshi haitoshi. 


Ayatollah amelihutubia taifa masaa kadhaa baada ya kushambulia kambi hizo za kijeshi.

Shambulizi hili ni la kisasi dhidi ya mauaji ya jenerali wa kikosi maalumu cha Quds cha Iran, Qassemi Soleimani aliyeuliwa na Marekani mjini Baghdad Ijumaa iliyopita. 

Khamenei amesema uwepo usio halali wa Marekani kwenye ukanda huo unatakiwa kumalizwa akisema umesababisha vita, mgawanyiko na uharibifu. 

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohamad Zarif amesema shambulizi hilo ni sawa na hatua za kujilinda huku rais wa halmashauri ya Ulaya Ursula von der Leyen akitoa mwito wa kufanyika makubaliano ya kidiplomasia.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post