MAREKANI YAMUUA KWA KOMBORA KAMANDA MKUU WA KIKOSI CHA QUDS CHA JESHI LA IRANI


Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) Meja Jenerali Qassem Solaimani na naibu mkuu wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq, al Hasdul Shaabi, Abu Mahdi al Muhandes wameuawa shahidi mapema leo Ijumaa katika shambulizi la roketi lililofyatuliwa na helikopta ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq.

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad mapema leo umeshambuliwa kwa maroketi ya helikopta za Marekani. Maafisa wa Marekani wamekiri katika mahojiano yao na shirika la habari la Reuters kwamba, shambulizi hilo limefanyika dhidi ya watu wawili wenye mfungamano na Iran.


Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Javad Zarif, ametaja hatua hiyo kuwa "hatari na uchokozi wa kishenzi".

Gen. Soleimani alikuwa mtu mashuhuri kwa utawala wa Iran. Kikosi chake cha Kikurdi kilikuwa kinaripoti moja kwa moja kwa kiongozi mkuu wa kidini wa Iran Ayatollah Ali Khamenei na alisifiwa kama shujaa wa kitaifa.

Rais wa Marekani Donald Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter picha ya bendera ya Marekani baada ya kutangazwa kuuawa kwa jenerali hiyo.

Bei ya mafuta duniani imepanda kwa asilimia nne baada ya shambulio hilo.

Ripoti za vyombo vya habari vya Marekani zinasema kuwa Jenerali Soleimani na maafisa wa waasi wanaoungwa mkono na Iran nwalikuwa wakiondoka katika uwanja wa ndege wa Baghdad kwa kutumia magari mawili wakati waliposhambuliwa na ndege za Marekani zisizokuwa na rubani karibu na eneo kuweka mizigo.

Kamanda huyo aliripotiwa kusafiri kutoka Lebanon au Syria. makombora kadhaa yaliripotiwa kushambulia msafara wao, ambapo karibu watu watano wanaaminiwa kuawa.

Taarifa iliyotolewa na Pentagon ilisema: "Kufuatia agizo la rais, vikosi vya jeshi la Marekani vilichukua hatua ya kuwalinda wafanyikazi wake nje ya nchi kwa kumuua Qasem Soleimani,"

"Hatua hii ililenga kudhibiti mipango ya Iran ya mashabulio ya siku zijazo. Marekani itaendelea kuchukua hatua madhubuti kuwalinda watu wetu na maslahi yetu kote duniani," ripoti hiyo iliendelea kusema..

Pentagon inasema jenerali Soleimani aliidhinisha mashambulio dhidi ya ubalozi wa Marekani.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post