Picha : TAASISI YA HUDEFO NA WADAU MBALIMBALI WA MAZINGIRA WAFANYA USAFI UFUKWE WA MSASANI


Taasisi isiyo ya Kiserikali ya HUDEFO kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ambao wanamapenzi ya mazingira wamefanya usafi katika ufukwe wa Msasani ikiwa ni sehemu yao ya kufanya hivyo kila mwezi. Mratibu wa zoezi hilo Bi.Sarah Pima alisema kuwa wameamua kufanya hivyo kwa sababu wananchi wenyewe ndio haswa watumiaji wa ufukwe huo wa bahari, hivyo ni jukumu lao kuhakikisha inakuwa safi kila wakati.
Hali ya taka ngumu ilivyokuwa kabla ya kuanza usafi wa ufukwe wa bahari, ambapo pameonekana kuwa na tatizo kubwa hasa katika chupa za plastiki zenye rangi kusambaa bila kuokotwa kwa sababu hazina dili lolote kwa wale waokota makopo, hii inapelekea kuchafua bahari kwa kasi.
Wadau mbalimbali wakiendelea kusafisha ufukwe wa Msasani 
Moja ya kikundi cha wakimbiaji ambao hutumia pia ufukwe huo wa Bahari kwa ajili ya mazoezi yao ya kila wakati wakiwa wanafanya usafi
Wanafunzi kutoka Chuo cha NIT ambao wanapenda mazingira wakiwa wameungana na wadau wengine kuendelea kufanya usafi
Mratibu wa zoezi la usafi wa ufukwe wa Msasani Bi. Sarah Pima (aliyevaa buti la kijani) akitoa maelezo kwa wadau wa mazingira namna bora ya kukusanya taka hizo.
Ukusanyaji wa taka ngumu na zile ambazo zinaoza ukiwa unaendelea 
Kujali Afya ni muhimu hapa washiriki wa usafi wakiwa wanapewa vitendea kazi 
Wadau wa mazingira kwa uwezo wao wakiwa wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuondoa taka ngumu ambazo ni tatizo katika bahari
Baadhi ya taka ngumu ambazo zimeokotwa tayari kwa ajili ya kwenda kutupwa eneo maalumu.
Baadhi ya wanachuo kutoka UDSM wakiwa wanaendelea na usafi
Wadau wa mazingira wakiwa wanachimba mashimo ili kufukia taka ambazo zinaweza zikaoza
Hawa ni wadau wa mazingira ambao walifanikisha kwa kiasi kikubwa kufanya usafi katika ufukwe wa Msasani.

(Picha zote na Fredy Njeje - Mdau wa Mazingira)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527