MLEMAVU AWEKA RECORD KUKWEA MLIMA MERU


Mkurugenzi wa shirika la Mwanangu Development Tanzania (MWADETA), Walter Miya akiwa katika picha ya pamoja na watalii Ina Aakerberg toka Sweden na Santo (Mtanzania) baada ya kufika ‘Little Meru’ na kuweka record kwa walemavu kupanda mlima huo. (Imeandaliwa na Robert Okanda)
Sehemu ya watalii 21, wakiwemo watatu wenye ulemavu wa mgongo wazi waliotumia baiskeli na mmoja wa kutembea kwa miguu wakiwa katika picha ya pamoja walipofika 'Little Meru Mkoani Arusha hivi karibuni. 
Mkurugenzi wa shirika la Mwanangu Development Tanzania (MWADETA), Walter Miya akimsaidia Santosi Chuwa miongoni mwa vijana waliozaliwa na ulemavu wa mgongo wazi aliyefanikiwa kupanda ‘Little Meru’ katika ziara hiyo. 
Wahudumu wakiwajibika kumsaidia mtalii Ina Aakerberg kupanda mlima Meru. Alifanikiwa kufika ‘Little Meru’ Mita 3820 tofauti na wenzake kutokana na ujasiri wake uliomwezesha kutambaa, kutembea kwa magongo na hata kusukuma baiskeli yake kwa kuzungunsha magurudumu mpaka akatoboa kutimiza ndoto za kufika kilele cha mlima huo. 
Ina Aakerberg akisaidiwa kupanda mlima Meru hadi kufika ‘Little Meru’ Meta 3820. 
Wahudumu wakimsaidia mtalii Lisa Lebuser kupita eneo korofi waliotembelea Mlima Meru kuendelea na safari wakitokea kudhuru Mli huo. Kushoto ni Askari wa Arusha National Park, Dominic Shigangio. 
Ina Aakerberg (kulia) akipongezana na mwenzake Lisa Lebuser baada ya kufanikiwa kuvuka katika eneo korofi wakiwa safarini kupanda mlima Meru. 
Wahudumu wakiwajibika kumsaidia mtalii Ina Aakerberg kupanda mlima Meru. aliyefanikiwa kufika ‘Little Meru’ Mita 3820 tofauti na wenzake kutokana na ujasiri wake uliomwezesha kutambaa, kutembea kwa magongo na hata kusukuma baiskeli yake kwa kuzungunsha magurudumu mpaka akatoboa kutimiza ndoto za kufika 'Little Meru'. 
Ina Aakerberg akionesha furaha yake kwa wahudumu wa watalii walihusika katika kukokota baiskeli yake alipopanda Mlima Meru na kufanikiwa kuweka recodi ya kuwa mlemavu wa mgongo wazi na kichwa kikubwa aliefika kilele cha ‘little Meru’ mkoani Arusha hivi karibuni. Pamoja naye ni mama yake Mzazi Liiso Aakerberg na Mtalii mwingine kutoka Ujerumani, na washiriki wengine waliopanda mlima huo. 
Sehemu ya watalii wakiwa katika picha ya pamoja kwenye maanguko ya maji wakati wa kushuka Mlima Meru hivi karibuni. 
Wahudumu wakiwajibika kuhakikisha David Lebuser anapanda Mlima Meru japo hakufanikiwa kulifika ‘Little Meru’ kama ilivyokuwa kwa Ina Aakerberg kutoka na uchovu, uzito mkubwa pia changamoto ya miundombinu. 
Sehemu ya watalii 21, wakiwemo watatu ulemavu wa mgongo wazi waliotumia baiskeli na mmoja wa kutembea kwa miguu wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza safari ya kupanda mlima Meru hivi karibuni. 
Sehemu ya watalii wakifurahia mandhari ya mlima Meru wakati wa kushuka siku ya nne ya ziara hiyo. 
****
Kwa mara ya kwanza katika historia Ina Aakerberg mlemavu wa mgongo wazi kutoka nchini Sweden ameweka record kwa kutimiza ndoto ya maisha yake alipofanikiwa kupanda mlima Meru kwa baiskeli ya matairi matatu na kufika ‘Little Meru’ mita 3820 mwishoni mwa wiki. 

Binti huyo mwenye miaka 33 alipania kupanda mlima huo ili aweke historia kwa lengo la kuchangia ujenzi wa majengo ya kuhudumia wagonjwa wa migongo wazi na vichwa vikubwa hapa nchini Tanzania. 

Yeye pamoja na watalii wengine takribani 21 waliliapanda mlima huo ambao ni wa pili kwa urefu nchini kwa lengo la kutunisha mfuko wa kuchangia fedha za ujenzi wa jengo la kuhudumia wagonjwa wa vichwa vikubwa na migongo wazi kwenye hospitali ya Haydom Mkoani Manyara.

‘Tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kufanikiwa kupanda mlima na washiriki wote walifanikiwa kupanda mlima isipokuwa wawili kutoka Ujerumani wenye uelmavu wa migongo wazi walioshia kambi ya Miriakamba kutokana na chnagamoto za kiafya, alisema Mkurugenzi wa Shirika la Mwanangu Development Tanzania (MWADETA), Walter Miya.

Kwa kiasi kikubwa malengo yametimia kwa safari yetu tuliyokadiria kupata shilingi milioni 40 hata hivyo malengo yalifikiwa japokuwa bado mahitaji ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya huduma na malazi ni makubwa kwa sasa. 

“Tumefanikiwa kupata takribani milioni 50 hivi lakini tutaendelea na kufanya shughuli za kutunisha mfuko ili tufikie malengo mapana ya kupata jengo la vyumba vinne vya kulaza wagonjwa na kuwapatia huduma zingine mbalibali za mahitaji yao maalum” Alifafanua Dkt. Theresa Harbaur kutoka Ujerumani anayehudumia watoto kwenye hospitali ya Haydom Mkoani Manyara.

Tukio hilo la kihistoria lilidhaminiwa na makampuni mbalimbali chini ya usimamizi wa Shirika la Mwanangu Development Tanzania (MWADETA).

Mlima Meru una mita 4566 mpaka kileleni kutokea usawa wa Bahari.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527