ELIMU JUU SEKTA YA MADINI INATAKIWA MOROGORO


 Waziri wa Madini Doto Biteko kushoto akizungumza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro  Loata SanareWaziri wa Madini Doto Biteko katikati akizungumza, kushoto ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Sanare wakiwa kwenye kikao.


 Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akizungumzaNa Tito Mselem DodomaWaziri Biteko ameagiza uongozi wa Mkoawa Morogoro kwa kushirikiana na Wizara ya Madini kuandaa maonesho ya madini kwalengo la kuelimisha Umma kwa watu wa Morogoro na mikoa jirani juu yaSheria, Kanuni na fursa zilizopo katika Sekta ya Madini.Hayo yamebainishwa leo January 08, 2020 na Waziri wa Madini Doto Biteko alipofanya kikao na MkuuwaMkoawa Morogoro, LoataSanare, kilichofanyika katika ukumbi wa WizarayaMadini, Mtumba Jijini Dodoma.“Nichukue fursa hii kuwaelekeza wataalamu wote wa Wizara ya Madini na Taasisi zake kuhakikisha wanashirikiana naMkoa wa Morogoro kuzitangaza fursa zinazopatikana katika Sekta ya Madini Mkoani Morogoro kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo kuandaa maonesho yatakayopelekea kuelimika kwa wananchi wa Mkoa huo,” alisema Waziri Biteko.Aidha, Waziri Biteko amesisitiza ushirikiano katika kusimamia Sekta ya Madini kati yaWizara na Mkoa wa Morogoro na kumpongeza Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Morogoro Emmanuel Shija kwa kazi nzuri anazozifanya katika ukusanyaji wa mapato ya serikali.Waziri Biteko amesema maendeleo ya Sekta ya Madini katika Mkoa wa Morogoro yatatokana na wachimbaji wenyewe, hivyo Wizara na Mkoa inapaswa kuwalinda nakuwalea wachimbaji na wadau wote wa madini mkoanihumo.Akizungumzia changamoto inayowakabili wananchi wa Morogoro Biteko alisema ni pamoja na uelewa mdogo walionao juu ya masuala yanayohusiana na Sekta ya Madini kuwa ni kikwazo katika kupelekea maendeleo Mkoani humo.Kwa upande wake,Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, ameonesha kufurahishwa na kitendo cha Mkoa wa Morogoro kuonesha mafanikio makubwa katika makusanyo ya mapato ya serikali kutoka shilingi 811,714,294.12 kwa mwaka 2017/2018 mpaka kufikia 1,031,865,068.41 kwamwaka 2018/2019.“Madini ya Ujenzi, Vito na Dhahabu tukiyasimamia vizuri hakika yatatuingizia fedha nyingi watu wa Morogoro, hivyo nikuombe Mkuu wa Mkoa ukalifanyie kazi hilo, pia sisi kama Wizara ya Madini tutashirikana na Mkoawa Morogoro kuhakikisha wawekezaji wanakuja kuwekeza katika Sekta ya Madini Mkoani Morogoro,”alisemaNyongo.Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Sanare, amemuomba Waziri kupatiwa ushirikiano katika kuitangaza Morogoro kuwani Mkoa wa Madini na sio kilimo peke yake.Pia Sanare, amesema, Mkoawa Morogoro una mpango wakufufua viwanda vya Ceramics vilivyokuwepo ili kuongeza matumizi ya madini ya viwandani yanayopatikana katika Mkoa huo kwa wingi na kuendeleza uhamasishaji wa uanzishwaji wa viwanda vipya vya Ceramics.Wakatihuohuo, AfisaMadiniMkaziwaMkoawa Morogoro, Emmanuel Shija,amesema Mkoawa Morogoro una Jumlaya leseni 3082 za wachimbaji wa dogo kati yake ni leseni 250 tu ndizo zinafanya kazi ya uzalishaji, hivyo Ofisi ya Madini inaendelea na zoezi la kufuta leseni zote zenye makosa.“Mwaka 2019 jumlayaleseni 223 zilifutwa na jumla ya hati za makosa kwa leseni 836 zimetolewa, leseni hizo ziko kwenye utaratibu wa kufutwa ndani ya mwaka huu wa fedha endapo wamiliki wa leseni hizo hawatarekebisha makosa yao kama Sheria inavyoelekeza,” alisemaShija.Kikao hicho kilicho lenga kujadili changamoto na maendeleo ya Sekta ya Madini kwaMkoa wa Morogoro ikiwa ni pamoja na kuangalia fursa zilizopo katika Sekta ya Madini katika kuharakisha maendeleo ya mkoa huo.

Ambacho kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Madini na Taasisi zilizo chini ya Wizara akiwepo Naibu Waziri waMadini, StanslausNyongo, Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini Prof. ShukraniManya, Mkurugenzi Taasisi ya Jiolojia na Utafiti Tanzania Dkt Musa Budeba, Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Madini Edwin Egenge, Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Madini Augustine Ollal na wengine.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post