KAMPENI YA TUMEBORESHA SEKTA YA AFYA YAHAMASISHA WADAU KUCHANGIA DAMU

 Afisa Habari wa Taasisi ya Chakula na Lishe Jackson Monela (wa kwanza kulia) akishiriki katika zoezi la kuchangia damu leo katika zoezi linaloendelea MOI ambapo wadau mbalimbali wamejitokeza.
Mtaalam wa Taasisi ya Tiba na Mifupa-MOI akishiriki zoezi la kutoa damu kwa mmoja wananchi waliojitokeza leo.
***

Na Andrew Chale 

KAMPENI ya Tumeboresha Sekta ya afya imeongeza  hamasa kubwa kwa Wananchi na wadau kujitokeza kwa wingi kuchangia damu ambapo sasa  Taasisi ya Tiba ya Mifupa-MOI inaweza kukusanya chupa za damu zaidi ya 150 kwa siku

Kampeni hiyo ambayo kwa mwaka huu ni awamu ya pili, imekuja kwa wakati muafaka ambapo wadau wa Asasi ya Family Federation  for World Peace  (FFWP) wamekuwa wakileta wachangia damu 1000 kwa siku.

"Tupo katika kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya. Ambapo pia tuliweza kutumia nafasi hii kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kuchangia damu hapa MOI na muitikio umekuwa mkubwa na tunapata damu kuanzia chupa zaidi ya 100 kwa siku na hii ni faraja kubwa sana kwetu" alisema Afisa Habari  na Mahusiano  MOI, Patrick Mvungi.

Mvungi aliongeza kuwa, Asasi hiyo ya FFWP imeshaleta wananchi 1500 huku siku ya kwanza ikileta wananchi 1000 na siku ya pili Wananchi 500 na  wanatatajia kumalizia 500 wengine.

Aidha. Mvungi amebainisha kuwa,  kwa upatikanaji huo wa damu kwa sasa hakuna mgonjwa anayekosa kufanyiwa upasuaji kwani kuna damu ya kutosha. 

"Mahitaji ya damu MOI  kwa siku ni chupa 15 hadi 30. Kabla ya zoezi ili la kuchangia damu, kwa siku  tulikuwa tunapata chupa chini ya 15  na zilikuwa zinatoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama na Wananchi wachache waliokuwa wanakuja kujitolea.

Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya inaendeshwa na Maafisa Habari waandamizi kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake ambapo kampeni hiyo itakuwa endelevu na Watanzania wanahamasishwa kujitokeza kuendelea kuchangia damu kwa wenye mahitaji.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527