PAPA FRANCIS AOMBA RADHI KWA KUMCHAPA KIBAO MUUMINI


Papa Francis ameomba radhi kwa kitendo chake cha kumchapa kibao, mmoja wa waumini kwenye kanisa la St Peter's Square huko Rome.

Papa alikuwa akisalimiana na watoto na mahujaji na wakati akigeuka mwanamke mmoja aliyekuwa kwenye umati wa watu waliokuwa karibu aliuvuta mkono wa Papa kwa nguvu karibu amuangushe.

Hali iliyomfanya Papa kugeuka na kumpiga makofi mawili mkononi mwanamke huyo kwa hasira.Papa akiwa anavutwa na muumini

Badaye Papa alikiri kwamba alishindwa kujizuia na yeye pia huwa anakosea kama binadamu wengine.

Hivyo anaomba radhi kwa kitendo hicho kwa muumini huyo na kila mtu.

Kitendo cha Papa cha kumzaba makofi ya mkononi mwanamke huyo, kimezua mjadala kwenye mitandao ya kijamii, hasa Twitter, wengi wakimuunga mkono Papa.

Awali wakati wa hotuba yake ya mwaka mpya, Papa alikemea unyanyasaji dhidi ya wanawake.



Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527