WAZIRI WA KILIMO: BODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO NI MUHIMU KISEKTA

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mwanza

WAZIRI wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga amesema Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ni mkombozi kwa wakulima hapa nchini.

Mhe. Hasunga ameyasema hayo jana tarehe 9 Disemba 2019 alipotembelea na kukagua maghala ya kuhifadhi nafaka na katika eneo la Mkuyuni Jijini Mwanza.

Amevitaka bodi hiyo kuwa ni mkombozi kwa wakulima kutokana na jukumu lake la kuhakikisha uzalishaji wa mazao ya nafaka unaongezeka kadhalika pia bodi hiyo inanunua mazao ya nafaka na kuyaongezea thamani.

Amesema kwa kuanzisha kiwanda Jijini Arusha cha kusaga nafaka na kuuza, huku kukiwa na dhamira ya  kujenga kiwanda cha kuchakata Alizeti na nafaka Jijini Dodoma itawanufaisha wananchi kwa kuuza bidhaa zilizotemgemezwa nchini tofauti na kuuza malighafi.

Amesema kuwa dhamira ya serikali kupitia Bodi hiyo mkoani Mwanza ni kujenga kiwanda cha kuchakata mpunga na mazao mengine hivyo bodi hiyo ni muhimu kisekta.

Mhe. Hasunga pia ameipongeza Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko kwa kutekeleza vema maelekezo ya Serikali ya kununua na kuuza Korosho.

“Moja ya Jukumu tulioipatia Bodi mwaka huu ni kununua na kuuza Korosho kwa niaba ya Serikali na kazi hiyo wameifanya vizuri, wameweza kunua Korosho yote na wanayo.” Alifafanua.

Alisema, Bodi kama wafanyabiashara imeweza kununua Korosho na kuongeza thamani (Ku- process) kwa kuziweka kwenye vifungashio vya viwango mbalimbali

MWISHO


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post