WAZIRI JAFO AMNYOOSHEA KIDOLE MKURUGENZI WA MOMBA...AMPA SIKU 30 | MALUNDE 1 BLOG

Monday, December 16, 2019

WAZIRI JAFO AMNYOOSHEA KIDOLE MKURUGENZI WA MOMBA...AMPA SIKU 30

  Malunde       Monday, December 16, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo ameonyesha kukerwa sana na utendaji wa kazi wa Mkurugenzi aa Halmashauri ya Wilaya ya Momba Mkoani Songwe kwa kushindwa kutekeleza miradi ya maendeleo ipasavyo.


Hilo limejitokeza leo hii tarehe 16 Desemba wakati Waziri huyo alipotembelea wilayani humo kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kuongea na watumishi.

Jambo lililo mkera zaidi Waziri huyo ni kitendo cha halmashauri hiyo kupokea fedha za mradi Mkakati wa ujenzi wa Soko la mazao la Kimataifa toka mwezi Septemba mwaka 2018 lakini hadi sasa ndiokwanza wapo katika umaliziaji wa jamvi.

Licha ya mradi huo lakini mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya umejengwa kwa kusuasua sana jambo ambalo limeonyesha dhahiri kwamba Mkurugenzi huyo haendani na kasi ya serikali ya awamu ya tano. Pia hadi sasa halmashauri imekusanya mapato kwa Wastani wa asilimia 24 toka kuanza mwaka wa fedha 2019/2020.

Jafo amempa mkurugenzi huyo siku 30 majengo ya soko yawe yamefikia hatua ya kupauwa lasivyo ataonyesha wazi kwamba kazi ya Mkurugenzi haiwezi.

Wakati huo huo Jafo amekagua jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa jengo hilo linalo jengwa kwa utaratibu wa Force Account.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post