WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM KUANDAMANA DESEMBA 19


Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso) imetoa saa 72 kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kutoa mikopo kwa wanafunzi waliokosa, vinginevyo wanafunzi watakutana nje ya ofisi za bodi hiyo zilizopo Mwenge Dar es Salaam Desemba 19, 2019.


Taarifa iliyotolewa jana Jumapili Desemba 15, 2019 na Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Daruso, Judith Mariki ilisema wamefikia uamuzi huo baada ya changamoto ya kukosekana kwa mikopo kwa wanafunzi wengi wa mwaka wa kwanza tangu chuo kifunguliwe huku baadhi ya wanafunzi wanaoendelea wakikatwa fedha zao.

Mariki alisema baada ya juhudi kubwa ya kufuatilia na mazungumzo kugonga mwamba, serikali imefanya mazungumzo ya ndani kwa ndani iliyojumuisha mihimili mitatu ya serikali hiyo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post