UPELELEZI KESI YA ALIYEMCHOMA MOTO MKE WAKE WAKAMILIKA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, December 31, 2019

UPELELEZI KESI YA ALIYEMCHOMA MOTO MKE WAKE WAKAMILIKA

  Malunde       Tuesday, December 31, 2019

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa upelelezi wa kesi inayomkabili Mfanyabiashara Khamisi Luwonga anaedaiwa kumuua Mkewe Naomi Marijani kwa kumchoma kwa kutumia gunia mbili za mkaa umekamilika.Wakili wa Serikali Mwandamizi Simon Wankyo ameyasema hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Salum Ally, wakati kesi hiyo ilipofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa, ambapo imepigwa kalenda hadi siku ya Januari 7, 2020, itakapotajwa tena.

Mfanyabishara huyo, anadaiwa kutenda kosa hilo Mei 15, 2019, nyumbani kwake maeneo ya Gezaulole Kigamboni, baada ya kumuua na kisha kumchoma moto wa magunia mawili ya mkaa mke wake na kisha kuyabeba mabaki ya mwili huo na kwenda kuyafukia shambani kwake Mkuranga.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post