MKURUGENZI TAN TRADE AWATAKA WANANCHI SINGIDA KUCHANGAMKA


Na Shushu Joel - Singida
Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bw. Edwin Rutageruka amewataka Wadau wa Alizeti wa Mkoa wa Singida kupanga mikakati ya pamoja ya kuongeza uzalishaji wa alizeti ili kutosheleza mahitaji makubwa ya viwanda vya kusindika alizeti ambavyo vinashindwa kuzalisha mafuta kwa mwaka mzima kutokana na kukosekana kwa malighafi.


 Bw. Rutageruka ametoa wito huo wakati akiongea na Wasindikaji, wakulima wa alizeti na watendaji wa Serikali wakati wa Mkutano na Wadau wa alizeti wa Mkoa wa Singida uliofanyika katika Ukumbi wa VETA.

 Mkutano huo umeandaliwa na TANTRADE kwa ushirikiano na Uongozi wa Mkoa wa Singida pamoja na Chama cha Wasindikaji wa Mafuta ya Alizeti Singida ( SISUPA) na kushirikisha Wadau wapatao 110 kutoka Mkoa wa Singida.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiwahutubia wadau wa alizeti wa Mkoa wa Singida wakati akifunga rasmi mkutano wa kupanga mikakati ya kuongeza uzalishaji wa alizeti kukidhi mahitaji ya viwanda vya kusindika alizeti kwa mwaka mzima.

 Pamoja na mambo mengine Mhe. Dkt Nchimbi ameelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya zilizopo Mkoani Singida wahakishe wanaondoa Tozo zinazosababisha kero kwa Wakulima, Wasindikaji na Wafanyabiashara ya alizeti.

Kikao hicho kilichofanyika Mjini Singida na kuhudhuriwa na Wadau zaidi ya 110 wakiwemo Wakulima, Wasindikaji, Wafanyabiashara, Viongozi wa Vyama vya Ushirika na Watendaji wa Serikali.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post