RAIS MAGUFULI ATUMIA SHEREHE ZA UHURU KUTANGAZA MAFANIKIO YA OPERESHENI ZA KUPAMBANA NA UVUVI HARAMU

Na Mwandishi Wetu,  Mwanza

RAIS Dk. John Pombe Magufuli ametumia Sherehe za 58 ya Uhuru kuelezaa mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia Sekta ya Uvuvi baada ya Serikali kuongeza mapambano dhidi ya Uvuvi Haramu na kuwezesha kuongezeka mapato kutoka Shilingi bilioni 379 mwaka 2016/2017 hadi kufikia shilingi bilioni 691 mwaka 2018/2019.

Akizungumza kwenye maadhimisho ya Uhuru yaliyofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Rais Magufuli amesema mapambano hayo ya uvuvi haramu yamewezesha pia kuongezeka kwa mavuno ya samaki kutoka tani 387,547 mwaka 2017/2018 hadi kufikia tani 448,474 mwaka 2018/2019.

Rais Magufuli amesisitiza kuwa vita dhidi ya uvuvi haramu imewezesha sasa wakazi wa Mikoa inayozunguka Ziwa Victoria kuanza kupata samaki wakubwa hali iliyowezesha ongezeko kubwa la mapato ya nchi yatokanayo na sekta ya uvuvi.

“Tumeongeza pia mapambano dhidi ya uvuvi haramu hali ambayo imesaidia upatikanaji wa samaki.. Kwa mfano kwenye mwaka 2018/ 2019 tulivuna tani 448,474 kutoka tani 387,547 mwaka 2017/2018”alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli alisisitiza kuwa hata wananchi wa mikoa inayozunguka Ziwa Victoria ni mashahidi wa mafanikio hayo ya operesheni za kupambana na uvuvi haramu kwani nao wanashudia ongezeko la samaki.

“lakini hata ninyi wana Mwanza ni mashahidi hivi sasa kwa mikoa hii ya Mara, Mwanza na Kagera kwamba samaki wakubwa wameanza kupatikana hii pia imesaidia kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka bilioni 379 mwaka 2016/2017 hadi kufikia sh bilioni 691 mwaka 2018/2019”alisema Rais Magufuli.

Pia Rais Magufuli alisisitiza kuwa kwa kutambua kuwa takribani asilimia 65 ya watanzania wanajihusisha na shughuli za Kilimo Uvuvi na Ufugaji Serikali imefuta zaidi ya tozo 100 kwenye sekta hizo.

Mbali na mafanikio hayo ya Opereshi za kupambana na Uvuvi haramu, Rais Magufuli pia amesema awamu ya awamu ya tano inaendelea kutatua migogoro ya ardhi ili kuwawezesha wananchi kuendelea na shughuli za Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ufanisi mkubwa.

“Tunashughulikia pia migogoro ya ardhi ikiwemo kuviruhusu vijiji 920 vilivyokuwa kwenye maeneo ya hifadhi kuendelea kuwepo”alisisitiza Rais Magufuli.

Wakizungumza kwenye viwanja wa Kirumba jijini Mwanza baadhi ya wakazi wa mikoa inayozunguka Ziwa Victoria wamekiri kuwepo ongezeko kubwa la samaki kutokana na usimamizi madhubuti wa Serikali kwenye rasilimali hizo.

Mmoja wa wananchi wa Mwanza Gaudensia  Maduka alisema kabla ya Rais Magufuli kuingia madarakani walikuwa wananunua samaki kilo moja kwa sh 7,00 lakini kutokana na juhudi za Serikali kudhibiti uvuvi haramu sasa wananunua kwa sh 4, 000 kwa kilo.

“Tunamshukuru sana Rais  Magufuli  kwa kazi nzuri aliyotufanyia wananchi wa Mwanza sasa tunajivunia kupata samaki wakubwa tena kwa bei nafuu…tunamuombea kwa Mungu amzidishie ujasiri na msimamo thabiti katika kulinda rasilimali za uvuvi kwani sisi kanda ya Ziwa uvuvi ndio maisha yetu”alisema Maduka.

Naye Mabula Malando alisema sasa hata biashara ya samaki imekuwa nzuri kwani wajasiriamali wengi wameingia kwenye biashara hiyo kutokana na upatikanaji wa samaki kuwa mkubwa na kupongeza juhudi za Rais Magufuli katika udhitibi wa Rasilimali hizo za Uvuvi.

Kwa zaidi ya miaka mitatu sasa Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekuwa ikiendesha operesheni za kupambana na uvuvi haramu katika maji yote ikiwemo Ziwa Victoria, Bahari ya Hindi, Ziwa Tanganyika, Ziwa Nyasa, Bwawa la Nyumba ya Mungu, Bwawa la Mtera ili kulinda rasilimali hizo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Kwa nyakati tofauti Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina alinukuliwa na vyombo vya habari ndani ya Bunge na nje ya Bunge akisisitiza msimamo wa Serikali katika kulinda rasilimali hizo za taifa na kuonya viongozi wanaojihusisha kufadhili uvuvi haramu kwa visingizio mbalimbali ikiwemo uchaguzi kuacha tabia hiyo kwani hawatapona.

Pia Spika wa Bunge, Job Ndugai wakati wa upitishaji azimio la Tanzania kudhiria mkataba wa kimataifa wa FAO wa kupambana na uvuvi haramu alisisitiza kuwa ni lazima rasilimali hizo zilindwe na doria kuendelea kwani rasilimali hizo zisipolindwa zitatoweka na kuleta hasara kubwa kwa taifa.

Ndugai alikwenda mbali zaidi na kuwaonya wanasiasa tutotumia rasilimali za uvuvi kuwashawishi  wananchi kuvunja sheria kwa minajili ya kutaka kuungwa mkono  na kwamba kama kuna tatizo la Sheria Bunge liko tayari kuirekebisha lakini sio 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post