MSHINDI WA PROMOSHENI YA TIGO CHEMSHA BONGO 2019 AKABIDHIWA GARI LAKE


Mkazi wa Zanzibar, Shaban Khamis Ali(49) akifurahia mara baada ya kukabidhiwa gari yake aina Renault Kwid yenye thamani ya 23m/- baada ya kuibuka mshindi wa promosheni ya Tigo Chemsha Bongo 2019.  
BAHATI IMEMUANGUKIA Mzee Shaban Khamis kutoka Zanzibar kushinda Gari aina ya Renault Kwid. Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani, Joseph Mutalemwa, amempongeza Mzee Shaban kwa kutumia fursa ya #TigoFiesta2019 Chemsha Bongo vizuri 
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani, Joseph Mutalemwa,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kumkabidhi zawadi Mshindi wa promosheni ya Tigo Chemsha Bongo 2019 
“Kuna vitu vikitokea kwenye maisha yako inakuwa ngumu kuficha hisia zako. Nashukuru TIGO kwa kuleta mchezo huu wa #TigoChemshaBongo nilicheza nikiamini nitashinda pesa lakini nimeambulia zawadi kubwa kabisa ya gari” ,Mzee Shaban Khamis
Dar es Salaam Desemba 5 2019.Mkazi wa Zanzibar, Shaban Khamis Ali(49) amekabidhiwa rasmi gari yake aina ya Renault Kwid yenye thamani ya 23m/- baada ya kuibuka mshindi wa promosheni ya Tigo Chemsha Bongo 2019.
Promosheni hiyo iliyodumu kwa siku 90 kuanzia tarehe 4 Agosti hadi 14 Novemba 2019 na wateja wa Tigo walipata nafasi ya kujishindia zawadi za pesa taslim kila siku na droo ya mwisho mshindi alikuwa anajinyakulia zawadi ya gari. Promosheni hii ilishuhudia washindi 90 kila siku waliojishindia Tshs 100,000 na washindi wengine 90 waliojishinda Tshs 50,000. Pia tuliwapa washindi 12 kili wiki kwa mda wa wiki 12, Tshs 1,000,000.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Shabaan alisema “Wakati napigiwa simu,nilikuwa nyumbani najipanga kutoka kuenda katika mihangaiko yangu ya kibiashara, basi nilipopata ile taarifa kwamba nimeibuka mshindi nilifurahi sana kwani sikutegemea kabisa kuwa ningeibuka mshindi katika promosheni hii, habari hizi naziona kama ndoto kwangu, nashukuru Tigo kwa kunifungia mwaka vizuri na kutimiza ndoto yangu ya kumiliki gari, kwani itanisaidia katika mizunguko yangu ya kibiashara “alisema kwa furaha.

Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani, Joseph Mutalemwa, alimpongeza mshindi huyo na kutumia fursa hiyo kuwashukuru wateja wote wa kampuni ambao walishiriki na baadhi yao kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi za fedha taslimu ambayo yalitolewa na kampuni hiyo.

“Tunayo furaha kubwa katika kipindi hiki tunachoelekea katika msimu wa sikukuu kumkabidhi mshindi wetu wa gari ya aina Renault Kwid,yenye thamani ya 23m/-, gari hili ni jipya kabisa,. Tunawashukuru wateja wetu nchi nzima walioshiriki kwenye promosheni hii ya miezi mitatu ambayo imemalizika mwishoni mwa mwezi wa Novemba 2019”,alisema Mutalemwa.

Aliongeza kuwa, promosheni hii ambayo ilianza jijini Mwanza katika msimu wa Tigo Fiesta 2019-Saizi Yako imepata mafanikio makubwa kutokana na wateja wengi kujitokeza kushiriki na baadhi yao kufanikiwa kujishindia zawadi(fedha taslim) mbalimbali na hivyo Tigo kufanikisha lengo lake ambalo lilikuwa ni kuwashukuru wateja kwa kuiunga mkono kampuni kupitia kununua bidhaa zake mbalimbali.

Mutalemwa aliwashukuru wateja wote wa Tigo kwa kuendelea kuunga mkono kampuni na kuahidi kuwa promosheni mbalimbali za kunufaisha wateja wa kampuni hiyo zinatendelea kubuniwa katika siku za usoni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post