ASKARI POLISI WALIOSUKA NYWELE ZA MITINDO WAAGIZWA KUZIFUMUA KABLA YA JANUARI 1,2020

Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Edward Mbugua, ameonyesha wasiwasi juu ya maafisa wa polisi waliOsukwa nywele zenye mapambo ya kuvutia jambo ambalo ni ukiukaji wa sheria.

Maafisa wote wa kike watalazimika kufumua nywele walizosukwa zisizoendana na sheria ya mavazi ya polisi kuanzia tarehe 1, 2020, kwa mujibu wa idara ya Polisi nchini Kenya.

"Kuna haja ya kutambua kwamba sare ya polisi ni ishara ya mamlaka na inastahili kupewa heshima yake. Kuanzia Januari 1, 2020, nywele za mitindo isiyokubalika hazitakubaliwa," Bwana Mbugua amethibitisha.

Maafisa wa kike wa polisi nchini Kenya watatakiwa kuondoa mitindo yao ya nywele pamoja na zile walizobandika katika kipindi hiki cha sikukuu.

Idara hiyo ya polisi inasema inataka kuhakikisha maafisa wote wanafuatilia kikamilifu mfumo wa mavazi rasmi ya kazi.

Aidha hatua hii inaenda sambamba na sare mpya za polisi zilizotolewa.

Taarifa iliyotolewa mapema wiki hii, inasema kwamba makamanda wote wa polisi wa eneo wamepewa jukumu la kuhakikisha kwamba sheria ya mavazi inafuatiliwa vilivyo.Inspekta Jenerali Mbugua amedai kuwa mitindo ya nywele zilizosukwa inafanya iwe vigumu kwa maafisa hao kuvaa kofia zao wakiwa kazini.

Taarifa hiyo iliyotiwa saini na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Edward Mbugua, ilionyesha wasiwasi kuhusu maafisa wa polisi walisukwa nywele zao zilizowekwa mapambo ya kuvutia na kukiuka mavazi rasmi ya polisi.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa Desemba 20, 2019, Bwana Mbugua anasema kwamba upambaji wa nywele kwa nakshi kupita kiasi ni ukiukaji wa kanuni za idara ya Polisi.

"Katika ziara yangu rasmi ya kikazi sehemu mbalimbali nchini katika kipindi cha wiki moja iliyopita, nimeshuhudia maafisa wa ngazi mbalimbali hususan wa kike wakiwa wamesuka nywele zao kwa namna isiyokubalika," Mr Mbugua amesema.

Kuanzia tarehe Mosi Januari, 2020, polisi wanawake nchini Kenya watatakiwa kufuata kikamilifu sheria na kanuni za mavazi ya polisi nchini huo.
Sare ya Polisi

Inspekta Jenerali Mbugua amedai kuwa mitindo ya nywele zilizosukwa inafanya iwe vigumu kwa maafisa hao kuvaa kofia zao wakiwa kazini.

Bwana Mbugua ameonyesha wasiwasi wake juu ya hijabu za rangi kwa Waislamu akikisitiza kwamba wanastahili kuvaa hijabu rasmi nyeusi ya kitambaa chembamba kulingana na sheria.

"Nimeshuhudia vazi la kuhifadhi kichwa kwa Waislamu lililobadilishwa kulinganisha na makubaliano ya awali yaani kutoka mtandio mweusi hadi ile yenye rangi," amesema.

Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527