MWALIMU MKUU ATIWA MBARONI NA TAKUKURU KWA RUSHWA YA NGONO KWA MWANAFUNZI ILI AMPE CHETI


TAKUKURU Mkoani Dodoma wanamshikilia Mkuu wa Shule ya Sekondari Serengeti iliyopo Serengeti Mkoani Mara, Baraka Sabi kwa tuhuma za kuomba rushwa ya ngono kwa Mwanafunzi aliyemaliza kidato cha sita katika shule hiyo ili ampatie cheti chake cha kuhitimu.

Akiongea na Waandishi wa Habari leo Jumapili,  Kamanda Wa Takukuru Mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo amesema wamemkamata Mkuu  huyo wa  shule kwa kushirikiana na Mwanafunzi aliyeombwa rushwa ya ngono Mkazi wa Dodoma ambaye alihitimu  mwaka 2016 na alikuwa anataka cheti aombee kazi  

“Mwalimu Baraka alimwambia Mwanafunzi asipate shida ya kwenda Serengeti yeye ana safari ya kuja Dodoma katika  Mkutano wa Wakuu wa Shule na atakuja na cheti, walipokutana akaomba rushwa ya ngono ndipo ampe cheti, Msichana akaomba udhuru na kuahidi kurejea, kisha akatutonya” -Amesema  Kibwengo 


Amesema baada ya kupokea taarifa hiyo waliweka mtego na kufanikiwa kumkamata akiwa na mtoa taarifa kabla yakufanya tendo hilo.

Amesema Takukuru walifanikiwa kuchukua cheti hicho na uchunguzi wa awali unaendelea kwa mujibu wa sheria na hatua stahiki zitachukuliwa baada ya kukamilika.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527