AFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMWA MAHARAGE


Watu watatu wamefariki dunia katika matukio matatu tofauti yaliyotokea wakati wa Sikukuu ya Krismasi katika Wilaya za Muleba, Bukoba na Ngara mkoani Kagera, akiwemo mtoto Everine Method mwenye umri wa miaka 13, mwanafunzi wa Shule ya msingi Kagoma, ambaye mwili wake ulikutwa kichakani.

Akizungumzia matukio yaliyotokea wakati wa Sikukuu ya Krismasi, Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi amesema kuwa tukio la kwanza lilitokea katika kijiji cha Kagoma wilayani Muleba.

Kamanda Malimi amesema kuwa mtoto huyo ametumwa na shangazi yake aliyekuwa akiishi naye, kwenda kuvuna Maharage kwa ajili ya mboga, lakini hakurejea hadi maiti yake ilipokutwa katika kichaka na Mzee Tryphone Katabaro aliyekuwa akichunga mbuzi.

Kuhusu tukio la pili Kamanda Malimi amesema kuwa Johan Japhet mwenye umri wa miaka 38, mwili wake uligundulika kandokando mwa njia katika Kijiji cha Nakatunga wilayani Ngara, na kuwa tukio la tatu ni la mtembea kwa mguu Pauline Karugira mkazi wa Mtaa Bugombe, katika Mansipaa ya Bukoba, aliyepoteza maisha baada ya kugongwa na chombo cha moto ambacho hakijafahamika kama ni pikipiki

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527