LIVERPOOL YABEBA TAJI LA KLABU BINGWA DUNIANI KWA MARA YA KWANZA


Liverpool wameibuka mabingwa wa kombe la Klabu Bingwa wa Dunia, baada ya kuifunga Flamengo ya nchini Brazil bao 1:0 katika mchezo wa fainali.
Roberto Firmino, mshambuliaji wa Liverpool ndo aliyefunga bao pekee la ushindi mbele ya timu ya Flamengo kwenye mchezo wa fainali ya kombe la klabu bingwa duniani.Firmino alifunga bao hilo ndani ya dakika za nyongeza baada ya dakika 90 kukamilika bila timu hizo kuonyeshana ubabe kwenye fainali hiyo ya kibabe.
Ushindi huo unaifanya Liverpool iliyo chini ya Jurgen Klopp kutwaa taji hilo la dunia kwa mara ya kwanza.


Liverpool imekua timu ya pili kutoka England kushinda ubingwa Wa Dunia kwa ngazi ya vilabu baada ya Manchester United kufanya hivyo mwaka 2008.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post