HATMA YA ERICK KABENDERA BADO IPO KWA DPP


Kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Mwandishi wa Habari za Uchunguzi, Erick Kabendera, imepigwa kalenda hadi Januari 2, 2020 itakaposikilizwa tena, ambapo upande wa utetezi, umeieleza Mahakama kuwa bado wanaendelea kufanya majadiliano na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP),kufuatia barua ya kukiri makosa yake aliyoiandika ili aweze kusamehewa.


Hayo yamejiri leo Disemba 18, 2019, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, wakati kesi hiyo ilipofikshwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa

Akizungumza mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo Janeth Mtega, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, amesema kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la ukwepaji wa Kodi, kuongoza genge la uhalifu pamoja na utakatishaji wa fedha zaidi ya shilingi milioni 170, makosa ambayo anadaiwa kuyatenda kati ya Januari 2015 na Julai 2019, maeneo mbalimbali ya Jiji hilo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post