HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA YAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS LA KUWALIPA FIDIA WANANCHI WALIOPISHA ENEO LA JESHI | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, December 1, 2019

HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA YAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS LA KUWALIPA FIDIA WANANCHI WALIOPISHA ENEO LA JESHI

  Malunde       Sunday, December 1, 2019
Na.Faustine Gimu Galafoni ,Dodoma

Halmashauri ya jiji la Dodoma imeshaanza kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli alilotoa Nov.25 mwaka huu la kulipa fidia kwa wananchi  1526 wanaopisha eneo la Jeshi la Wananchi Jijini Dodoma.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana  Nov.30,2019  jijini Dodoma  mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwin Kunambi amesema kiasi kinachotakiwa kulipwa kwa wananchi hao ni Tsh.Bil.3.399  na ukubwa wa eneo zima  ni ekari elfu tano  na eneo linalopaswa kulipwa fidia ni ekari  elfu 3 mia 4 na 31 na kinachotakiwa kwa wanufaika  ni kufungua akaunti za benki huku uhakiki ukiendelea.

Aidha,Bw.Kunambi amesema ofisi ya mkurugenzi  jiji la Dodoma imeshaanza kuwasaidia wananchi kusaidia kufungua akaunti za benki na kuanzia wiki ijayo wananchi wataanza kulipwa fedha zao.

Ikumbukwe kuwa Nov.25,2019 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli wakati akiweka jiwe la Msingi eneo la Jeshi la Ulinzi alitoa agizo kwa  halmashauri ya jiji la Dodoma kuwalipa fidia wananchi  1526 wanaopisha mradi wa eneo la jeshi la Ulinzi.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post