HALIMA MDEE ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA BARAZA LA WANAWAKE WA CHADEMA (BAWACHA)


Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amechaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha) baada ya kupigiwa kura 317 za ndio.

Katika uchaguzi huo ulioanza jana Alhamisi Desemba 12,2019 na kumalizika leo Ijumaa Desemba 13, 2019 Mdee alikuwa mgombea pekee kwenye nafasi ya uwenyekiti .

Matokeo ya Uchaguzi huo yametangazwa leo Disemba 13, 2019, ambapo kupitia ukurasa wa Twitter wa chama hicho ukatoa mchanganuo wa Mwenyekiti pamoja na Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara na Zanzibar.

"Mkutano Mkuu wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) ulioanza jana asubuhi, umemalizika asubuhi hii ambapo umemchagua Halima Mdee kuwa Mwenyekiti wa Bawacha Taifa" imeeleza taarifa hiyo.

Aidha katika Uchaguzi huo Hawa Mwaifunga, amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bawacha Tanzania Bara, huku Sharifa Suleiman, akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti Zanzibar.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post