CAG MSTAAFU PROF. MUSSA ASSAD ATOLEA UFAFANUZI MADAI YA KUTEKWA

Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Assad amekanusha taarifa zilizodai kuwa alikuwa ametekwa.

Akizungumza na Azam TV, Prof Assad amesema siku ambayo inadaiwa alichukuliwa na watu wasiojulikana, alikuwa kwenye hafla ya kidini wilayani Kisarawe.


""Tangu juzi nilipewa mwaliko wa siku tatu na watu wa Umoja wa Wanataaluma wa Kiislamu Tanzanzia (Tampro) kwenda kwenye warsha Kisarawe kuzungumzia namna ya kuhuisha taasisi hiyo na niliwaambia nitakuwapo kwa siku moja badala ya tatu," amesema Profesa Assad

Amesema alimuaga mke wake na kuondoka kwa kutumia gari yake aina ya GD Wagon mpaka Kisarawe na eneo husika lilikuwa mbali na hakukuwa na mtandao wa simu wowote unaopatikana.

“Niliingia pale saa 2 tumefanya shughuli ile mpaka nimemaliza kusaliisha pale saa 3 ndio nikatoka pale na muda nafika Kisarawe mjini simu zikaanza kuingia lakini mimi nikiendesha gari sipokei simu” amesema Profesa Assad

Amesema aliendesha hadi kufika maeneo ya Ukonga, Dar es Salaam kwenye taa za kuongoza magari barabarani kuna kijana wake akampigia simu na kuipokea.

“Nikamwambia nipo barabarani akasema basi hii inatosha acha niwaambie nyumbani, nikajua kuna shida nyumbani lakini hakukuwa na shida yoyote kwangu," amesema ProfesaAssad.


Msikilize hapo chini


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post