ASKARI JKT WADAIWA KUUA RAIA KWA KIPIGO | MALUNDE 1 BLOG

Monday, December 16, 2019

ASKARI JKT WADAIWA KUUA RAIA KWA KIPIGO

  Malunde       Monday, December 16, 2019

Polisi mkoani Rukwa inawashikilia vijana watano wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mwanakijiji Sabato Mbalamwezi baada ya vijana hao kuvamia Kijiji cha Kipande wilayani Nkasi na kutembeza kipigo kwa wanakijiji wakidai wameiba simu.


Inaelezwa kuwa Sabato Mbalamwezi na mwenzie Renatus Wankamba walikamatwa na kuhifadhiwa Kituo cha Polisi kwa tuhuma za kuiba simu yenye thamani ya Tsh 25000, na wakiwa kituoni hapo walifika Vijana watano wa JKT na kuanza kuwaadhibu wakiwatuhumu kuwa wameiba simu ya mwenzao mmoja, Sabato alizidiwa baada ya kipigo na akafariki muda mfupi baada ya kukimbziwa Zahanati.

“Baada ya Vijana wale wa JKT kuwaadhibu watuhumiwa hao wa wizi wa simu, huyu mmoja Sabato alizidiwa kwa kipigo na akafariki muda mfupi baada ya kukimbizwa Zahanati, Wanakijiji walichukizwa na tukio hilo na kuanza kuwashambulia JKT hao hadi mmoja akakimbizwa Hospitali.

“Vijana watano wa JKT waliosababisha kifo cha Mbalamwezi wanashikiliwa na Polisi kwa mahojiano na watafikishwa Mahakamani,pia Wanakijiji 35 waliofanya fujo kwa Vijana hao wa JKT wamehojiwa na kuachiwa kwa dhamana”- Amesema Jutine Masonje,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post