ALIYEACHIWA KWA MSAMAHA WA RAIS ATIWA MBARONI TENA BAADA YA KUVAMIA NYUMBA YA KULALA WAGENI NJOMBE ILI AIBE


Amiri Kilagalila-Njombe
Mtuhumiwa mmoja aliyefahamika kwa majina ya Mstafa Msola maarufu kwa jina la (Hitler) aliyeachiwa huru kwa msamaha wa Rais mkoani Njombe amekamatwa tena na kurudishwa rumande kwa tuhuma za kuvunja nyumba ya kulala wageni kwa minajili ya kuiba.



Akizungumza na vyombo vya habari mjini Makambako mkoani hapa,kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema Musa Msola ni mmoja wa wafungwa walioachwa huru siku ya jana mara baada ya msamaha wa Rais uliotolewa disemba 9 siku ya maadhimisho ya uhuru wa Tanganyika.

“Akiwa mkoani Njombe kwanza aliomba msamaha mbele ya mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkuu wa mkoa wa Njombe kuwa anawasihi wenzake wawe ni watu wema,lakini ni masaa nane yamepita mtuhumiwa huyu aliyekuwa huru ilifika majira ya  saa tisa usiku,alijikuta ameshawishika kwenda kufanya  tukio la uvunjaji,na alienda kuvunja gesti moja Nang’ano iliyopo mtaa we Mwembetogwa hapa Makambako,na kwa kuwa wananchi wanaelewa jukumu lao la ulinzi waliweza kupeana taarifa usiku ule na alikamatwa”alisema kamanda Hamis Issa

Kwa upande wake mtuhumiwa Mstafa Msola amesema anashindwa kujitetea kwa kuwa ameshawishika kufanya kosa hilo licha ya kuwa huru kwa msamaha wa Rais.

“Nimefanya kosa kubwa sana nashindwa kujitetea kutokana msamaha ulipotoka nilishkuru hivyo nimejikuta nimeingia tena kwenye kosa”alisema Mstafa

Mstafa Msola ni mmoja kati ya wafungwa 70 walioachiwa huru siku ya jana mkoani Njombe mara baada ya msamaha wa Rais akitokea gereza la Njombe lililoachia huru wafungwa 25.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527