YALIYOJIRI LEO MAHAKAMANI KATIKA KESI YA ALIYEMCHOMA MOTO MKEWE KWA MAGUNIA YA MKAA


Upande wa mashtaka katika kesi ya tuhuma za mauaji inayomkabili mfanyabiashara Khamis Luwonga anayedaiwa kumuua mkewe Naomi Marijani kwa kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa, umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  kuwa upelelezi wa kesi hiyo kuwa jarada la shauri hilo lipo kwenye hatua ya uchapaji.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon amedai hayo leo Novemba 18, mwaka 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Salum Ally, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Amedai shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa, na kwamba upelelezi umekamilika na  jarada lipo kwenye hatua ya uchapaji kwa ajili ya maandalizi ili lipelekwe kwa  Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) hivyo wanaomba tarehe nyingine ili waweze kufatilia suala hilo.

Hakimu Ally amearisha kesi hiyo hadi Desemba 2, mwaka huu. 


Mshitakiwa anadaiwa Mei 15, 2019 katika eneo la Gezaulole Kigamboni Dar es Salaam alimuua mkewe Naomi Marijani kisha kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa ambapo alichukua majivu ya marehemu na kwenda kuyafukia shambani kwake Mkuranga.

 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post