ASKARI POLISI, MTUMISHI WA MAHAKAMA KORTINI WAKITUHUMIWA KUPOKEA RUSHWA


Watu wawili akiwamo askari polisi ambaye ni mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam nchini Tanzania, Leslie Koini wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu wakikabiliwa na kosa la kuomba rushwa ya Sh200, 000.

Pia,  upande wa mashtaka umedai mshtakiwa ambaye ni karani wa mahakama hiyo Itialy Omary hakuwepo mahakamani hapo hivyo wameiomba mahakama hiyo hati ya kukamatwa mshtakiwa huyo.


Akizungumza leo Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustina Mmbando, Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Odessa Horombe amedai Mei 8, mwaka 2018 mshtakiwa Omary na Koini kwa pamoja walipokea rushwa ya Sh. 200,000 kutoka kwa Mussa Abdallah ikiwa kama kishawishi ili asikutwe na we na hatia katika kosa namba 211/2018 la usalama barabarani.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo mshtakiwa  alikubali kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka ulidai bado haujajiandaa hivyo wanaomba ahirisho la muda kwa ajili ya kujiandaa.

Hata hivyo, Hakimu Mmbando alitoa masharti ya dhamana kwa mshtakiwa ambapo alitakiwa kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua na vitambulisho halali atakayesaini bondi ya Sh. 500,000.

Mshtakiwa ametimiza masharti ya dhamana, nje kwa dhamana.Kesi hiyo itatajwa tena Novemba 21 mwaka huu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post