MKAPA AWEKA WAZI ROSTAM AZIZ ALIVYOCHANGIA KUANZISHWA NHIF


Rais mstaafu, Benjamin Mkapa ameweka wazi kuwa uamuzi wa kuwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ni mpango ulioasisiwa na mfanyabiashara maarufu nchini Rostam Aziz.

Katika kitabu chake cha ‘My Life, My Purpose’ alichokizindua wiki iliyopita jijiji Dar es Salaam, Mkapa ameeleza alijifunza mpango huo wakati mfanyabiashara huyo alipokuwa Mbunge wa Jimbo la Igunga alikouasisi mwaka 1996 kabla ya kutangazwa rasmi kuwa wa kitaifa.

“Njia nyingine ya moja kwa moja ya kuwasaidia masikini ni kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ambao umejitolea kuzipatia familia hizo bima za afya.

“Nilijifunza kuhusu mpango huu kutoka kwa Rostam Aziz, Mbunge na mmoja kati ya wafanyabiashara wakubwa waliofanikiwa.

“Mwaka 1996 alianzisha mpango wa bima ya afya kwa wananchi wake wa Jimbo la Igunga kwa kiwango kidogo cha fedha ya Sh 10,000 ambacho kilisaidia familia yenye watoto wanne kutumia bima hiyo kwa kipindi cha mwaka mzima. Tuliamua kuutangaza mpangohuu kitaifa,” ameeleza Mkapa katika kitabu chake hicho.

Amesema ingawa mpango huo ulipoanzishwa haukueleweka vizuri kwa watu kwani wengine walisema “sitaumwa sasa kwanini nitoe fedha yangu kwenye mfuko huu,” lakini waliendelea kusisitiza juu ya mpango huo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527