LUGOLA AMUAGIZA IGP SIMON SIRRO KUMCHUKULIA HATUA MBUNGE WA CHADEMA KWA KUMTIMUA MPANGAJI WAKE


Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Kangi Lugola amemuagiza IGP Simon Sirro kumchukulia hatua Mbunge Sophia Mwakagenda (CHADEMA), na wengine wanaotoa kauli zenye viashiria vya uvunjifu wa amani.

Mbunge huyo amesema amemuondoa mpangaji (Polisi) kwenye nyumba yake, kwa sababu haoni haja ya kushirikiana nae.

 
“Mimi Sophia Mwakagenda sina mtendaji wala sijui kiongozi gani niishipo nitakaefanya nae kazi mpaka muweke mambo yenu sawa, pia leo namtoa kwenye nyumba yangu mpangaji wangu ambaye ni askari polisi akakae huko anakolipwa mshahara, nyumba ni yangu,” alisema Sophia.



Akijibu kauli hiyo Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Kangi Lugola amesema;“Jeshi la Polisi Tanzania tumekwishajipanga kuhakikisha amani inakuwepo kuanzia urejeshwaji wa fomu, rufaa, kampeni mpaka uchaguzi wa serikali za mitaa na matokeo. Hakuna Mtanzania yoyote, kikundi ama chama cha siasa kitakachofanya fujo ama kuharibu mali watu wakati wa uchaguzi.

“Nina taarifa chama kimoja kimejiondoa kwenye uchaguzi, ni imani yangu kwamba chama hicho kinaweza kuwa na mpango wa kuvuruga uchaguzi. Ninawaambia kwamba, hakuna chama chochote cha siasa kitakachovuruga uchaguzi, tutatumia nguvu yoyote kuhakikisha hakuna uvunjifu wa amani.

“Kuna viashiria vya uvunjifu wa amani vimeanza kujitokeza kuanzia humu Bungeni kwa kuwafukuza wapangaji, nawasishangae tukianza kuchukua hatua,. Tutaanzia hapa Bungeni kuchukua hatua.

“Namuelekeza IGP Sirro kuanza kuchukua hatua kuanzia Mbozi na kwa Mbunge huyu (Sophia Mwakagenda) ambaye ameanza kuonyesha viashiria vya uvunjishu wa amani. Wasiijaribu serikali ya awamu ya Tano, tuko vizuri sana, kiberiti kimejaa njiti, wakitikisa kitawaka,” amesema Lugola.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527