WAUGUZI NA WAKUNGA WAPEWA MAFUNZO YA UANZISHAJI WA DAWA ZA KUFUBAZA MAKALI YA VVU – NIMART

Wauguzi na wakunga kutoka vituo vya afya,hospitali na zahanati mkoa wa Shinyanga wamepatiwa mafunzo ya uanzishaji wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI (Nurse Initiated Management of Anti – Retroviral Therapy – NIMART) ili waweze kuwahudumia watu wanaoishi na maambukizi ya VVU na UKIMWI. 

Mafunzo hayo yatakayodumu kwa muda wa siku 10 yameanza leo Jumanne Novemba 19,2019 katika ukumbi wa Karena Hoteli Mjini Shinyanga na kukutanisha pamoja wauguzi 28 kutoka halmashauri zote za mkoa wa Shinyanga waliosajiriwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania (TNMC). 

Mafunzo hayo yameandaliwa na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto kwa kushirikiana na TAMISEMI pamoja na Asasi ya kitaifa isiyo ya kiserikali ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) inayojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya UKIMWI na UKIMWI. 

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo,Afisa Muuguzi kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mark Ogweyo amesema yanalenga kuwajengea uwezo wauguzi na wakunga nchini ili waweze kuwahudumia watu wanaoishi na maambukizi ya VVU na UKIMWI,ikiwemo kuwaanzia dawa za kufubaza makali ya VVU. 

“Kupitia mafunzo hayo wauguzi na wakunga watasaidia kwa kiasi kikubwa kuiwezesha nchi kufikia malengo ya 90-90-90 ya VVU na UKIMWI ifikapo mwaka 2020 ambapo lengo ni kuhakikisha watu wanapima VVU, kutumia dawa na kufubaza makali ya VVU”,alisema Ogweyo. 

“Tunataka ifikapo mwaka 2020, asilimia 90% ya watu wenye maambukizi ya VVU wamefikiwa na kupimwa,ambapo asilimia 90% ya walioapata maambukizi watapewa dawa za kufubaza virusi (antiretroviral treatment) na asilimia 90% ya watakaotumia dawa hizo hawataweza kuwaambukiza wenza watakaojamiiana nao kwa sababu virusi vitakuwa vimefubazwa na tiba hiyo,alieleza Ogweyo. 

Kwa upande wake,Mratibu wa Mafunzo kutoka AGPAHI,Violet Rugangila aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kuhakikisha wanatumia ujuzi watakaopewa ili kuhakikisha nchi inafikia malengo ya 90-90-90 huku akiwakumbusha wauguzi na wakunga kutoa elimu ya kutosha kwa wateja kabla ya kuwapatia dawa za kufubaza makali ya VVU.
Afisa Muuguzi kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Mark  Ogweyo akizungumza wakati wa mafunzo ya uanzishaji wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI (Nurse Initiated Management of Anti – Retroviral Therapy – NIMART) kwa wauguzi na wakunga kutoka halmashauri za wilaya ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde 1 blog
Afisa Muuguzi kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mark  Ogweyo akielezea kuhusu malengo ya 90-90-90 ya VVU na UKIMWI ifikapo mwaka 2020.
Afisa Muuguzi kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mark Ogweyo akisikiliza swali kutoka kwa mshiriki wa mafunzo hayo.
Wauguzi na wakunga kutoka vituo vya afya,hospitali na zahanati mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya uanzishaji wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI – NIMART.
Wauguzi na wakunga wakijadiliana wawili juu ya umuhimu wa  uanzishaji wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI.
Mratibu wa Mafunzo kutoka AGPAHI,Violet Rugangila akizungumza wakati wa mafunzo ya uanzishaji wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI (Nurse Initiated Management of Anti – Retroviral Therapy – NIMART) kwa wauguzi na wakunga kutoka halmashauri za wilaya ya Shinyanga. 
Mratibu wa Mafunzo kutoka AGPAHI,Violet Rugangila akizungumza  wakati wa mafunzo ya uanzishaji wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI.
Washiriki wa mafunzo wakifanya Mtihani wa kupima uelewa wa washiriki kabla ya mafunzo hayo.
Wauguzi wakifanya Mtihani wa kupima uelewa wa washiriki kabla ya mafunzo hayo.
Wauguzi wakifanya Mtihani wa kupima uelewa wa washiriki kabla ya mafunzo hayo.
Wauguzi wakifanya Mtihani wa kupima uelewa wa washiriki kabla ya mafunzo hayo.
Wauguzi wakifanya Mtihani wa kupima uelewa wa washiriki kabla ya mafunzo hayo.
Afisa Muuguzi kutoka Chuo cha Operating Theatre Management Mbeya, Samwel Mwangoka akikusanya mitihani ya kujipima kwa washiriki kabla ya mafunzo.
Afisa Muuguzi kutoka Chuo cha Operating Theatre Management Mbeya, Samwel Mwangoka  na Afisa Muuguzi Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza,Sarah Bipa wakiwa ukumbini.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
Afisa Muuguzi Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza,Sarah Bipa akitoa mada kuhusu malengo ya 90-90-90.
Afisa Muuguzi Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza,Sarah Bipa akitoa mada ukumbini.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527