WANNE WAHUKUMIWA KUNYONGWA KWA KUMUUA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA


Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza imewahukumu kunyongwa hadi kufa washtakiwa wanne kati ya saba waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza (RPC), Liberatus Barlow.

Hukumu hiyo imetolewa jijini Mwanza jana  Jumanne Novemba 12, 2019 na Jaji Sirialus Matupa baada ya Mahakama kuridhika bila shaka yoyote na ushahidi uliowasilishwa na washtakiwa walitenda kosa hilo.

Waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa ni Muganyizi Michael, Magige Mwita, Abdallah Petro na Abdulrahaman Ismail.

Walioachiwa huru na Mahakama baada ya ushahidi kutowatia hatiani katika kesi hiyo ya mauaji namba 192/2014 ni Chacha Mwita, Buganizi Edward na Bhoke Marwa.

Kamanda Barlow aliuawa kwa kupigwa risasi katika tukio lililotokea eneo la Kitangiri Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza saa 8:00 usiku wa kuamkia Oktoba 13, 2012.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527