WAFADHILI MIRADI YA TAFITI ZA SAYANSI WAKUMBUSHWA KUFUATA VIPAUMBELE VYA NCHI KWANZA


Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dr. Amos Nungu (kushoto) akizungumza na waandishi jijini Dar es Salaam, kulia ni Mratibu wa mkutano wa sayansi Theophilus Mlaki.

Na Hellen Kwavava- Dar es Salaam

Wafadhili wa Miradi ya tafiti za Sayansi kutoka nje ya nchi wametakiwa kufuata vipaumbele vya nchi husika kwanza ili kuwa na matokeo chanya ya tafiti hizo.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia nchini(COSTECH) Dr. Amos Nungu baada ya kumaliza majadiliano ya siku kwenye Mkutano wa baraza la wanasayansi,Teknolojia na Ubunifu unaoendelea jijini Dar es Salaam kwa wiki nzima.

Dr Nungu amesema wakati huu wanaangalia sana kupokea ufadhili ambao utaweka malengo ya nchi mbele kwanza kuliko kufanyia kazi tu malengo ya wafadhili.

“Kwa sasa tunaona ipo haja kwa wafadhili kuruhusu kuwa na malengo yetu kwanza katika miradi hiyo na yao kufuata ili nchi yetu nayo tufikie kwenye malengo ambayo tumejiwekea kwanza katika tafiti nchini”,amesema Nungu. 

Aidha Dr. Nungu amesema kuwa ushirikishwaji ulio wazi na usawa katika tafiti mbalimbali kwa nchi zilizoshiriki mkutano huo utaleta matokeo chanya na yenye kukuza maendeleo zaidi.

“Lazima maendeleo ya kitafiti na ubunifu yaonekane kwa jamii hasa wa nchini ili kuleta usawa ambao utakuwa na matokeo ya chanya ambayo jamii itaweza kuweka uaminifu katika sayansi",ameongeza Dr. Nungu.

Hata hiyo ameiomba serikali kuwekeza kwa asilimia 100 kwenye tafiti za kisayansi ili kuondoa changamoto zilizopo zinazokwamisha tafiti hizo kufanyika kikamilifu.

”Bado kuna changamoto kubwa ya miundombinu ya kitafiti mama maabara za kisasa kwa nchi nyingi za Afrika Kama serikali zetu zikiwekeza kikamilifu katika tafiti basi changamoto hizo zitaweza kuondoka”.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post