WAKE WA VIONGOZI WAKIONGOZWA NA MAMA JANETH MAGUFULI WATOA MISAADA KITUO CHA WAZEE NUNGE KIGAMBONI

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli ameungana na wake wa viongozi mbalimbali katika kusherehekea miaka 10 ya umoja wao uitwao New Millenium Women’s Group kwa kutoa misaada katika kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.

Mama magufuli, ambaye aliambatana na Mlezi wa umoja huo Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Magufuli, Mwenyekiti wake Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mama Tunu Pinda na Mama Asina Kawawa aliungana na wajumbe hao kutoa misaada mbali mbali ya ujenzi, chakula na nguo.

Mama Magufuli alichangia jumla ya gypsum 178 huku Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akituma mchango wa shilingi milioni 5 kwa ajili ya ukarabati wa Bwalo la kituo hicho kikongwe ambacho hadi leo Novemba 15, 2019 kilikuwa na wazee 26.

Umoja huo wa New Millenium Women’s Group ulichangia ujenzi wa mnara wa kisima cha maji kwa gharama ya shilingi milioni 1.9, vyakula na nguo vyenye thamani ya shilingi milioni 3.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa na wajumbe wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New Millenium Women’s Group akiwasili katika kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo. Wengine toka kushoto ni Mama Tunu Pinda, Mama Mary Majaliwa, Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Elimu, sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na Mama Asina Kawawa.
Wajumbe wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New Millenium Women’s Group wakiwa katika kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo walikofika kutoa misaada mbalimbali katika kuadhimisha umoja huo
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitoa misaada ya nguo na vyakula kwa kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa akitoa misaada ya nguo na vyakula kwa kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli katika picha ya pamoja na wajumbe wenzie wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New Millenium Women’s Group na baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigamboni katika kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli katika picha ya pamoja na wajumbe wenzie wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New Millenium Women’s baada ya kukabidhi misaada katika katika kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli katika picha ya pamoja na wajumbe wenzie wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New Millenium Women’s na wakaaazi wa kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiagana na wajumbe wenzie wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali uitwao New Millenium Women’s baada ya kukabidhi misaada katika katika kituo cha kulea wazee cha Nunge Kigamboni jijini Dar es salaam leo. PICHA NA IKULU

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post