Picha : MAHAFALI YA 33 CHUO CHA VETA SHINYANGA YAFANA.... WAHITIMU WASHAURIWA KUJIAJIRI WENYEWE


Na Marco Maduhu - Malunde 1 blog
Chuo Cha Ufundi Stadi (VETA) mkoa wa Shinyanga, kimefanya Mahafali ya 33, huku wahitimu wakishauriwa kujiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali ili wapate mikopo na kujiajiri wenyewe, kuliko kukaa mitaani na kusubiri ajira na wakati ujuzi wanao wa kuwapatia kipato na hatimaye kuendesha maisha yao.


Mahafali hayo yamefanyika leo Novemba 15, 2019 kwenye viwanja vya chuo hicho, huku mgeni rasmi akiwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA) Flaviana Kifizi.

Akizungumza kwenye Mahafali hayo,Kifizi amewataka wahitimu hao kujiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali ili waweze  kupata fedha za halmashauri za mapato ya ndani asilimia 10, ambazo hutolewa kwa vijana asilimia nne, ili wapate mitaji na kujiajiri wenyewe kuliko kupoteza ujuzi wao kwa kusubiri kuajiriwa na kuanza kulalamika maisha magumu.

“Natoa wito kwa wahitimu wa fani mbalimbali ambao mnahitimu leo muache tabia ya kutegemea kuajiriwa, bali mjijenge kujiajiri wenyewe kwani  ujuzi mnao,muutumie kujipatia kipato na kuinuka kiuchumi,” amesema Kifizi.

“Pia mjiunge kwenye vikundi vya ujasiriamali ili mpate mitaji na kufungua ofisi zenu na kujiajiri wenyewe, kuliko kumaliza masomo yenu hapa na kuishia kukaa mitaani na kulalamika hakuna ajira na wakati ujuzi mnao,”ameongeza.

Katika hatua nyingine amewataka wafanyabiashara kuchangamkia fursa ya kujenga hosteli jirani na chuo hicho cha Veta, ili kuondoa changamoto ya wanafunzi kupanga kwenye Magheto na kuambulia ujauzito, pamoja na wengine kuwa watoro sugu na kuacha masomo.

Akisoma Risala kwa niaba ya wahitimu wenzake Magreth Edward  amesema changamoto kubwa ambayo hukabiliana nayo ni ukosefu wa ajira, huku wakiomba Serikali kulegeza masharti ya upataji wa mikopo asilimia nne kwa vijana ili wapate kujiunga kwenye vikundi na kupata mitaji ya kujiajiri wenyewe.

Amesema wakati wanaanza kusoma mafunzo walikuwa 142, lakini wamehitimu wanafunzi 118, huku wanafunzi 24 wakishindwa kumaliza masomo yao kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo utoro sugu pamoja na wengine kuambulia ujauzito na kuacha masomo sababu ya kuishi kwenye Magheto.

Aidha mratibu wa mafunzo chuoni hapo Rashid Ntahigiye, amesema wanafunzi hao 118 wamehitimu fani mbalimbali ikiwemo umeme, uselemala, uchomeleaji, ubunifu na ushonaji nguo, ufundi bomba, ujenzi pamoja na mafundi wa mitambo.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi Veta mkoani Shinyanga Magu Mabelele, amesema chuo hicho kina jumla ya wanafunzi 400, wasichana 133 na wavulana 267, huku akitoa wito kwa wazazi wa Shinyanga kupeleka watoto wao chuoni hapo ili wakapate ujuzi ambao utatimiza ndoto zao.


TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA) Flaviana Kifizi akizungumza kwenye Mahafali ya 33 ya Chuo cha Ufundi Stadi (Veta) Mkoani Shinyanga. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Kaimu mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mkoani Shinyanga Magu Mbelele akisoma taarifa ya chuo hicho na kumkaribisha mgeni rasmi.

Mratibu wa mafunzo wa chuo cha Veta mkoani Shinyanga Rashid Ntahigiye akisoma taarifa ya chuo.

Mwanafunzi Magret Edward akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wenzake.

Wahitimu wakiwa kwenye Mahafali.

Wahitimu  wakiwa kwenye Mahafali.

Wahitimu wakiwa kwenye Mahafali.

Wahitimu wakiwa kwenye Mahafali.

Wahitimu  wakiwa kwenye Mahafali.

Wahitimu wakiwa kwenye Mahafali.

Wazazi wakiwa kwenye Mahafali.

Wazazi wakiwa kwenye Mahafali.

Wazazi wakiwa kwenye Mahafali.

Wazazi wakiwa kwenye Mahafali.

Wazazi wakiwa kwenye Mahafali.

Wazazi wakiwa kwenye Mahafali.

Wageni waalikwa na baadhi ya walimu wa chuo cha Veta wakiwa kwenye Mahafali.

Awali Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA) Flaviana Kifizi akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhitimu wa fani ya ushonaji Magreth Edward namna wanavyoshona nguo wenyewe.

Mwalimu Yona Mwambopa akimwelezeaMkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA) Flaviana Kifizi namna wanavyofundisha fani ya ukataji na ung'arishaji wa madini ya Vito.

Mwanafunzi Suzana Obed akikata madini ya Vito.

Kaimu mkuu wa chuo cha Veta Magu Mabelele akimwelezea mgeni rasmi Mkurugenzi wa SHUWASA Flaviana Kifizi namna wanavyofundisha fani ya utengezaji wa magari kwa njia ya mitambo.

Wanafunzi wakitoa burudani na kuonyesha mitindo mbalimbali ambayo wamebuni na kushona wenyewe.

Burudani ya kuonyesha mitindo ikiendelea kutolewa.


Burudani ya kuonesha mitindo ikiendelea kutolewa.

Burudani  ikiendelea kutolewa

Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA) Flaviana Kifizi akigawa vyeti kwa wahitimu.

Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA) Flaviana Kifizi akigawa vyeti kwa wahitimu.

Mgeni Rasmi  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga Mjini (SHUWASA) Flaviana Kifizi akigawa vyeti kwa wahitimu.




Awali wahitimu wakiingia ukumbini 

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527