UTEUZI MPYA ULIOFANYWA NA RAIS MAGUFULI LEO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Buruhani Salum Nyenzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA).

Dkt. Nyenzi (Tanzania Bara) anashika wadhifa huo kwa kipindi cha pili.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Dkt. Makame Omar Makame kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TMA.

Dkt. Makame (Zanzibar) ni Mhadhiri Mwandamizi wa Jiografia katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi hao umeanza tarehe 18 Novemba, 2019.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527