UNDER THE SAME SUN YAKUTANA NA WANAWAKE WENYE UALBINO,WANAWAKE WENYE WATOTO WENYE UALBINO MWANZA


Na George Binagi-GB Pazzo, Mwanza

Shirika la Under The Same Sun linaloshughulika na utetezi wa haki za watu wenye ualbino Tanzania limetoa mafunzo kwa wanawake wenye ualbino pamoja na wanawake wenye watoto wenye ualbino mkoani Mwanza ili kuwajengea uwezo kuhusu hali ya ualbino.
Mafunzo hayo ya siku tatu yameanza Novemba 22, 2019 jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Mfuko wa Kanada kwa ajili ya Mipango ya Kijamii (Canadian Fund for Local Initiative- CFLI) unaotekelezwa katika mikoa ya Mwanza na Shinyanga.

Mratibu wa mradi huo, Grace Wabanhu amesema matarajio baada ya mradi huo wa miezi minne kufikia tamati ni wanawake hao kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu hali ya ualbino na hivyo kuwa na ujasiri wa kuielimisha jamii inayowazunguka ili kuondokana unyanyapaa na ukatili dhidi ya watu wenye ualibino na hatimaye kuleta usawa katika jamii.


Naye Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ualbino (TAS) Mkoa Mwanza, Alfred Kapole amesema akina mama ni jeshi kubwa hivyo baada ya kuelimishwa kupitia mradi huo watakuwa mabalozi wazuri wa kutoa elimu katika jamii kuanzia ngazi ya nyumbani na hatimaye kusambaa hadi vijijini.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo mama mwenye mtoto aliye na ualbino, Shika Madebe kutoka wilayani Misungwi wameahidi kuitumia vyema elimu watakayoipata kwa kuwaelimisha wanajamii wengine ambao bado hawana uelewa wa kutosha kuhusiana na ualibino na hivyo kuondokana na unyanyapaa dhidi ya watu wenye ualibino ambao wamekuwa wakiitwa majina mabaya.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Tazama Video hapa chini

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527