MTENDAJI MKUU WA KAMPUNI YA MBOLEA NCHINI (TFC) ASIMAMISHWA KAZI | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, November 13, 2019

MTENDAJI MKUU WA KAMPUNI YA MBOLEA NCHINI (TFC) ASIMAMISHWA KAZI

  Malunde       Wednesday, November 13, 2019

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, amesema Serikali imemsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mbolea nchini (TFC), pamoja na kumuagiza Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya BAJUTA kuzirudisha haraka iwezekanavyo, fedha za umma kiasi cha Shilingi Bilioni 4.5.

Naibu Waziri Bashe ametoa kauli hiyo leo Bungeni Dodoma, wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Chunya, Victor Mwambalaswa, lililokuwa likihoji nini hatma ya mbolea na viuatilifu vya zao la korosho, ambavyo licha ya Serikali kutoa pesa ni mwaka sasa umepita mbolea na viuatilifu hivyo bado viko bandarini. 

Akijibu swali hilo Bashe amesema; “Ni kweli Serikali ilitoa pesa Bilioni 10 kwa ajili ya kuagiza viuatilifu hivyo na Serikali imemsimamisha Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya TFC kama hatua ya awali kwa uzembe huu”.

 “Nitumie nafasi hii ndani ya Bunge hili kuagiza Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bajuta kurudisha Bilioni 4.5 alizopewa na tumeongea na TPA wamekubali kutuondolea gharama zote na sasa tuko katika hatua za mwisho kuvitoa viuatilifu hivyo kabla havijaharibika ili tuweze kuwagawia wakulima” Bashe.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post