MVUA YAUA WATU 9 SENGEREMA JIJINI MWANZA

Watu tisa wa familia mbili tofauti katika Kata Yanyatukala Wilayani Sengerema, mkoani Mwanza wakiwemo wanawake wanne pamoja na watoto watano ambao nyumba zao ziko kwenye mkondo wa mto wamefariki, baada ya kusombwa na maji ya mvua.

 
Mvua hiyo iliyoanza kunyesha majira ya asubuhi, ilinyesha na kusababisha maafa kwa baadhi ya nyumba ambazo zipo pembezoni mwa mto na kupelekea nyumba hizo kusombwa na maji, kusababisha vifo vya watu tisa pamoja daraja kukatika na kusababisha kukosekana kwa mawasiliano.

Mkuu wa wilaya hiyo Dkt. Emmanuel Kipole amewataka wananchi wanaoishi katika maeneo hayo kuyapisha na kwenda kuishi katika maeneo ya muda, ambayo tayari serikali imeyabainisha ili kuepusha madhara zaidi.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella  ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mwanza, amewataka wakazi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari ili kuepusha kupoteza maisha ya wananchi wengine zaidi..

Miili yote ilikuwa imepatikana na imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Sengerema, baada ya zoezi la uokoaji kufanywa na wananchi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutumia nyavu na kamba.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527