WASHINDI WA 'PAKA NA USHINDE' WAJINYAKULIA ZAWADI | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, November 10, 2019

WASHINDI WA 'PAKA NA USHINDE' WAJINYAKULIA ZAWADI

  Malunde       Sunday, November 10, 2019


Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Rangi ya Plascon Tanzania, imewazawadia washindi mbalimbali wa promosheni ya 'Paka Rangi na Ushinde'.

Promosheni hiyo sasa imefikia wiki ya tano, ambayo hadi sasa washindi 21 wamepatikana na kujishinda sh. milioni 1 kila mmoja.

Promosheni hiyo ilikuwa imepokea zaidi ya washindi 1,000 kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Rangi ya Plascon Tanzania, Hussein Jamal, alisema:“Tukiwa kama kampuni tulianza rasmi shindano hili Oktoba, kiukweli tumepata mwitikio mzuri. Promosheni ya Paka Rangi na Ushinde imethibitisha kuwa kampuni yetu hurudisha kwa uaminifu au fadhila kwa wateja wetu”.
Jamal pia alisema promosheni hiyo inaonesha jinsi gani Plascon inavyotimiza wajibu wake kwa Watanzania pamoja na dhumuni lao la kuongeza thamani ya soko la rangi kupitia bidhaa yao, katika  ubora, uvumbuzi na kuwa suluhisho la rangi kwa watanzania. 
Promosheni hiyo iliyopewa jina la 'Paka Rangi na Ushinde', ilianza Oktoba na itafikia ukomo Desemba 14 na kuwavutia mamia na maelfu kwa kila mshiriki kuwa na uhakika wa kujipatia muda wa maongezi wa sh.500 na bado anakuwa na nafasi ya kushinda sh. milioni moja. 
Plascon hutoa zawadi ya sh. milioni 5 kila wiki kwa washindi mbalimbali.
Jamal aliongeza washiriki wanatakiwa kununua lita 20 ya rangi ya Plascon, na utapata utapewa kadi utakayoikwangua na kutuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenda namba 15054, ili kuwa katika nafasi ya kushinda. 

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post