CHADEMA WAITAKA SERIKALI KUTOTUMIA JINA NA NEMBO YA CHAMA CHAO KWENYE UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, November 10, 2019

CHADEMA WAITAKA SERIKALI KUTOTUMIA JINA NA NEMBO YA CHAMA CHAO KWENYE UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

  Malunde       Sunday, November 10, 2019

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetaka Serikali kutotumia nembo na jina la chama hicho kwenye karatasi za kupigia kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, mwaka huu.

Naibu Katibu Mkuu (Bara), wa chama hicho, John Mnyika amesema amesema hayo leo Jumapili Novemba 10, jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema sababu ya uamuzi huo ni kutokana na wao kujiengua katika kinyang’anyiro hicho hivyo wagombea wao wasiwepo katika fomu hizo za kupigia kura.

“Kesho Novemba 11, tutamuandikia barua Waziri wa Tamisemi (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Suleiman Jaffo, kuacha kutumia jina nembo ya chama chetu.

“Pia tunamuomba Rais Dk. John Magufuli, kuingilia kati ukiukwaji wa sheria unaoendelea kwenye uchaguzi huo kama alivyohamasisha wakati wa uandikishaji,” amesema Mnyika.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post