ATUPWA JELA KWA KUMPIGA NGUMI MBWA WAKE HADI KUFAJon Luc McLoughlin,aliyehukumiwa wiki 16, upande wa kulia ni Mbwa wake aliyemuua

Jon Luc McLoughlin, mwenye umri wa miaka 26, toka Poole Dorset nchini Uingereza, amehukumiwa kwenda jela wiki 16, baada ya kumpiga ngumi Mbwa wake hadi kufa.

Hukumu hiyo ilisomwa jana Novemba 28, 2019 na kuhudhuriwa na wanaharakati 25 wa Wanyama, pamoja na Mama yake mzazi na wadogo zake wawili.

Baada ya kuhukumiwa mdogo wake anayefahamika kwa jina la Alec Mackay, amedai kuwa hukumu ya wiki 16 ni ndogo na angetakiwa afungwe angalau mwaka 1. 

“Ingekuwa Binadamu angefungwa kifungo cha muda mrefu sana, kwakuwa sisi wote ni viumbe hai angeongezewa kifungo kidogo.”ameeleza Alec.

Matthew Knight, Mwendesha Mashtaka wa Haki za Wanyama nchini humo (RSPCA - Royal Society for the Prevention of Cruelty to Animals), amesema kuwa Jon alimpiga ngumi Mbwa wake hadi kufa na kumtupa karibu na mtaani kwao.

Mahakama ya Poole imepata taarifa kuwa Jon-Luc McLoughlin, alikaa na Mbwa huyo kwa Mwezi 1 pekee na hatimaye kumuua huku chanzo kikitajwa kuwa ni matatizo binafsi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post