MTOTO WA MIEZI MITANO ATELEKEZWA NYUMBA YA KULALA WAGENI NJOMBE


Na Amiri kilagalila-Njombe
Jeshi la polisi mkoa wa Njombe limefanikiwa kumpata mtoto wa miezi mitano aliyetelekezwa nyumba ya kulala wageni na kumuhifadhi chini ya uangalizi wa idara ya ustawi wa jamii.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa ametoa taarifa hiyo kwa wanahabari mkoani humo akibainisha kuwa mtoto huyo amekutwa kwenye nyumba ya kulala wageni inayofahamika kama Shamba Guest House iliyopo mjini Njombe huku akiacha ujumbe wa kuelekea mwanza .

“Shamba Guest amekutwa mtoto ambaye ana umri mdogo zaidi na ametelekezwa na mwanamke ambaye ni mama yake na ameacha ujumbe amesema anaenda eneo la Mwanza na huyu msaidizi amemuachia huyo mtoto,na pindi mambo yatakapo kuwa mazuru atamtumia hela”anasema Hamis Issa

Kwa mujibu wa kamanda mwanamke huyo anafahamika kwa jina la Stella Mtweve na mtoto huyo wa kiume mwenye umri wa miezi mitano na nusu  ametambuliwa kwa jina la Kelvin Mmagoma .


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post