MBUNGE AZZA HAMAD,MADIWANI WAKUTANA NA WANAWAKE WA MWAKITOLYO KUKOMESHA BIASHARA YA NGONO 'CHEMSHA CHEMSHA'

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akiongozana na madiwani 11 wanawake wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wamekutana na wanawake na mabinti wanaoishi katika kata ya Mwakitolyo ili kuzungumza nao namna ya kukomesha vitendo vya baadhi ya mabinti wenye umri kuanzia miaka 12 na wanawake watu wazima wanaofanya biashara ya kuuza miili yao maarufu ‘Chemsha chemsha’ ambapo wanaume hununua ngono kwa kupanga foleni.

Hatua ya mbunge na madiwani hao kukutana na wanawake na mabinti wa Mwakitolyo leo Jumatatu Novemba 18,2019 inatokana na azimio la kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kilichofanyika Mwezi Agosti mwaka huu ambapo Mhe. Azza aliomba aongozane na madiwani wanawake kwa ajili ya kwenda kuzungumza na mabinti na akina mama ili kukomesha biashara ya ngono katika kata hiyo.

Akizungumza katika kikao cha ndani na wanawake hao wakiwemo wanaomiliki gesti na nyumba za kupanga kilichofanyika katika kijiji cha Nyaligongo,Mhe. Azza amesema biashara ya ngono ni chafu inadhalilisha utu wa mwanamke lakini pia kuwaweka katika hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa mbalimbali ya zinaa hivyo inapaswa kupingwa na kila mtu.

“Ndugu zangu biashara ya ngono ni biashara ya kujidhalilisha naomba wanawake na mabinti wanaofanya biashara hiyo kuachana nayo. Tutafute kazi za kufanya ambazo siyo za kujidhalilisha,kazi yeyote ukiipenda na ukaifanya kwa moyo mmoja ni lazima utafikia malengo yako”,amesema Azza.

“Acheni biashara hii.Wanawake tutambue heshima tuliyopewa na mwenyezi Mungu,mama ndiyo anayejua kila kitu katika nyumba,mama ndiye aliyebeba majukumu makubwa katika familia,kwa hiyo tunatakiwa tuibebe heshima tuliyonayo badala ya kufanya biashara hii chafu ya kujidhalilisha”,alisema mbunge huyo.

Mhe. Azza ametumia fursa hiyo kuwataka wamiliki wa nyumba za kulala wageni ‘gesti’ na wanaopangisha vyumba kutoruhusu watu wanaofanya biashara ya kuuza miili kupanga kwenye vyumba.

Aidha amewashauri kuunda vikundi vya ujasiriamali na kuvisajili ili waweze kupata mikopo inayotolewa na halmashauri kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu na kwamba hata kama wana biashara zingine basi wajishughulishe pia na kilimo ili wawe na uhakika wa chakula katika familia zao.

“Nitumie fursa hii kumpongeza mtendaji wa kata ya Mwakitolyo na mashirika yasiyo ya kiserikali kwa kwenda kuwatafuta wanawake na mabinti waliokuwa wanafanya biashara na kuwapa elimu ya kuondokana na biashara hiyo na kuwapatia vyerehani ili waweze kufanya biashara ambayo ni halali,jambo ambalo limesaidia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa biashara hiyo”,ameongeza Azza.

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad(aliyefunga kitambaa cheupe katikati) akipokelewa na umati mkubwa wa wanawake akiwasili katika kata ya Mwakitolyo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga leo Jumatatu Novemba 18,2019. Picha zote na Said Nassor - Malunde 1 blog
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad(aliyefunga kitambaa cheupe katikati) akipokelewa na umati mkubwa wa wanawake akiwasili katika kata ya Mwakitolyo.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad(aliyefunga kitambaa cheupe katikati) akipokelewa na umati mkubwa wa wanawake katika kata ya Mwakitolyo 
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akipokelewa katika kata ya Mwakitolyo.

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza na wanawake wa kata ya Mwakitolyo.
Wanawake wa Mwakitolyo wakimsikiliza Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza na wanawake wa kata ya Mwakitolyo.
Afisa Mtendaji wa kata ya Mwakitolyo Samson Lutonja akisoma taarifa ya kata ikiwemo biashara ya Chemsha chemsa
Mbunge wa Azza Hilal na madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakisikiliza taarifa ya kata ya Mwakitolyo.
Diwani wa kata ya Mwakitolyo Limbe Augustine Limbe akizungumza katika kikao hicho.
Akina mama wakiwa kwenye kikao hicho.
Diwani wa viti maalumu Chausiku Hassan akizungumza katika kikao hicho.
Wanakikundi wakisoma risala mbele ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad 

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akimkabidhi Afisa Mtendaji wa kata ya Mwakitolyo Samson Lutonja Eploni 50 kwa ajili ya Mama Lishe katika kata ya Mwakitolyo.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza na baadhi ya mama lishe baada ya kuwakabidhi Eploni nyekundu zitakazowasaidia kwenye kazi yao.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza na baadhi ya mama lishe waliohudhuria kikao cha ndani cha mbunge,madiwani wanawake wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akipiga picha ya pamoja na Mama lishe pamoja viongozi wa halmashauri na kata.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akipiga picha ya pamoja na viongozi wa chama cha wachimbaji wadogo wanawake kata ya Mwakitolyo.Chama hicho kimemuomba Mbunge kuwa Mlezi wa chama  hicho.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akipiga picha ya pamoja viongozi wa kikundi cha hiari ya Moyo kijiji cha Nyaligongo kata ya Mwakitolyo kinachojihusisha na kuweka na kukopa.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akipiga picha ya pamoja viongozi wa kikundi cha hiari ya Moyo kijiji cha Nyaligongo kata ya Mwakitolyo.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akipiga picha na kikundi cha wanawake na maendeleo kilichoanzishwa kwa lengo la kuwafanya akina mama kuachana na biashara ya kuuza miili yao.Dhamira ya kikundi hicho ni kushusha Punda 200 'ndoo za mawe ya dhahabu' ili kusafisha senga 'mchanga wa dhahabu" 

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akiagana na akina mama wa Mwakitolyo.

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akiagana na akina mama wa Mwakitolyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post