JIMBO LA KIEMBESAMAKI KUENDESHA ZOEZI LA UPIMAJI KISUKARI BURE KWA WAZEE, NOVEMBA 14 | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, November 13, 2019

JIMBO LA KIEMBESAMAKI KUENDESHA ZOEZI LA UPIMAJI KISUKARI BURE KWA WAZEE, NOVEMBA 14

  Malunde       Wednesday, November 13, 2019


Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki, Mahmoud Thabit Kombo

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.

JUMUIYA ya Watu wanaoishi na ugonjwa wa Kisukari kwa kushirikiana na Madaktari wao wanatarajiwa kuendesha zoezi la upimaji ugonjwa huo kwa Wazee wa jimbo la Kiembesamaki tukio litakalofanyika kesho Novemba 14.

Zoezi hilo linaratibiwa na ofisi ya Mwakilishi wa jimbo hilo, Mahmoud Thabit Kombo ambaye ametoa wito kwa Wazee kujitokeza kwa wingi asubuhi na mapema kwenye Skuli ya Kiembesamaki A ambapo mbali na upimaji pia masuala mbalimbali ya kitaalamu ikiwemo ushauri vyote vitatolewa bure.

"Kambi hii maalum ya kupima Afya kwa Wazee ni katika kusherehekea siku ya Kisukari duniani. Naomba Wazee wote wajitokeze kwa wingi kesho siku ya Alhamisi ya kupima ugonjwa huu wa  kisukali" alieleza Mahmoud Thabit Kombo.

Aidha, Mahmoud Thabit Kombo ameongeza kuwa, amekuwa na utaratibu wa mara kwa mara kupeleka huduma muhimu zikiwemo za upimaji ili kusaidia wananchi kujua Afya zao.

"Mbali na zoezi la upimaji Kisukari. Pia kutakuwa na kambi zingine za magonjwa mbalimbali na Madaktari bingwa watafika kutoa huduma bure hii ni kuthamini afya za wananchi wetu" alimalizia Mahmoud Thabit Kombo.

Ugonjwa wa Kisukari umetaarifiwa kuwa ni miongoni mwa magonjwa hatari hivyo jamii imetakiwa kuepuka ikiwemo kuzingatia aina ya maisha pamoja na ufanyaji wa mazoezi.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post