KAMPUNI YA BUSINET AFRICA YADHAMIRIA KUENDELEZA ZAO LA ALIZETI MKOANI SINGIDA

 Meneja wa Mradi wa Kampuni ya BusinetAfrika Irene Njovu, akizungumza na waandishi wa habari mjini Singida jana, katika kikao cha wadau wa zao la alizeti kilichofanywa na kampuni hiyo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo.
 Kikao kikiendelea .
Meneja wa Mradi wa Kampuni ya BusinetAfrika Irene Njovu, Irene Njovu, akisisitiza jambo kwenye kikao hicho.Na Waandishi Wetu, Singida

KAMPUNI ya BusinetAfrica imedhamiria kuwasaidia Wakulima Mkoani Singida namna ya Kutengeneza maandiko ili waweze kupata mikopo kwenye Mabenki itakayowasaidia katika shughuli za kilimo. 

Kampuni hiyo imewakutanisha pamoja viongozi wa vyama vya ushirika kutoka kila wilaya za mkoa huo, wakulima wa zao la alizeti na wasindikaji wa zao hilo kwa lengo la kuwaunganisha  na taasisi za Kifedha ili waweze kufanya kazi kwa pamoja. 

Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kikao hicho Meneja wa Mradi wa Kampuni hiyo,  Irene Njovu alisema kampuni hiyo imekuja na mradi wa kuwasaidia wakulima wa zao la alizeti  kupata mikopo kwa kuwaunganisha na Benki ya Kilimo na Maendeleo Tanzania (TADB) kuwaelekeza taratibu zinazotakiwa ili waweze kupata mikopo. 

"Tumekuja na mradi wa kuendeleza zao la Alizeti Mkoa wa Singida na tumeamua kuwaunganisha wakulima na taasisi za kifedha hususani benki yao ili waweze kupata mikopo katika msimu huu wa kilimo". alisema  Njovu. 

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika 'SIFACU' Mkoa wa Singida, Yahaya Hamis alisema kutokana na wakulima wengi pamoja na Viongozi wa vyama vya ushirika kutokujua kuandika maandiko ili kupata mikopo,  kwa kupitia mradi huo watakuwa na ufahamu na kuanza kuandika maandiko yatakayosaidia kupata mbegu bora na kuongezeka uzalishaji wa zao hilo. 

Hata hivyo wakulima wameshukuru kwa hatua hiyo lakini hofu yao wameona mradi huo umechelewa, hivyo wameomba taasisi za kifedha hususani Benki ya Kilimo na Maendeleo Tanzania (TADB) ambayo ndio wameunganishwa nayo kutoa mikopo mapema ili waweze kupata mbegu bora kwa wakati kabla msimu haujaisha, huku wasindikaji wakiwa na matumaini ya kupata malighafi ya kutosha baada ya mradi huo kuwafikia. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post