KAMATI YA RUFAA ISIFUNGWE NA MAAMUZI YA WASIMAMIZI

Nteghenjwa Hosseah, Iringa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameelekeza  Kamati za Rufaa za Uchaguzi kutofungwa na maamuzi yaliyofanywa na Wasimamizi/wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi katika maeneo yao.

Jafo ameyasema hayo Mkoani Iringa wakati wa muendelelezo wa ziara yake Mikoani kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Tar 24/11/2019.

Katika kikao hicho na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Kamati ya Rufaa pamoja wasimamizi wa Uchaguzi ngazi za Wilaya Mhe. Jafo ameelekeza Kamati za Rufaa kutofungwa na maamuzi yaliyofanywa na Wasimamizi/Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wakati wa zoezi zima la Uteuzi.

“Wasimamia wa Uchaguzi wamefanya kwa nafasi yao kwa kadiri walivyoona inafaa sasa ni wakati wenu kuyachambua na kujiridhisha na kazi waliyoifanya maamuzi yao sio ya mwisho ninyi ndio mnatakiwa mtoe maamuzi ya mwisho katika malalamiko yatakayowasilishwa” Alisema Jafo

Nimelisema hili na naendelea kusisitiza nendeni mkafanye kazi kwa weledi na mkazingatie haki mkamalize malalamiko yote yatakayowasilishwa kwenu ili wagombea wawe na amani na Uchaguzi ufanyike salama alisisitiza Jafo.

“Rufaa iwe rufaa kweli kweli yaan mlalamikaji akifikisha malalamiko yake kwenu apate suluhisho la malalamiko yake, fanyeni maamuzi yenu kwa kuzingatia haki” Alisema Jafo.

Aliongeza kuwa msiwe na mashaka katika kazi yenu, mjiamini na mkatende kwa  weledi, mkapitie malalamiko yote kwa makini mkiona mtu anastahili mrudisheni kwenye kinyang’anyiro msifumgwe na maamuzi ya wasimamizi angalieni uhalisia wa malalamiko anayestahili mpeni na asiyestahili msimpe.

Wakato huo huo Waziri Jafo aliitaka Kamati ya Ulinzi na Usalama kuhakikisha wanalinda amani wakati wote wa Uchaguzi.

Waziri Jafo anaendelea na ziara yake katika Mikoa na Njombe, Morogoro na Tanga.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527