JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU YA DAR LADAI KUMUUA JAMBAZI SUGU | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, November 7, 2019

JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU YA DAR LADAI KUMUUA JAMBAZI SUGU

  Malunde       Thursday, November 7, 2019

Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam limedai kufanikiwa kumuua jambazi maarufu aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu anayejulikana kwa jina la Kambale, usiku wa kuamkia  Novemba 6, 2019, eneo la Ukonga Mazizini, jijini humo na kumkuta na silaha moja aina ya Bastola.


Taarifa hiyo imetolewa  Novemba 6, 2019, na Kamanda wa kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa imesema kuwa, jambazi huyo alikuwa ni maarufu sana kutokana na matukio yake ya utekaji wa bodaboda na kuwaua watu.

"Katika juhudi zetu za kupambana na uhalifu, tumeua jambazi maarufu sana alikuwa anaitwa kambale, ametesa sana kule Ukonga - Mazizini na Kinyerezi, amekuwa anateka watu na kuwaua bodaboda na kufanya chochote anachotaka na jina la Kambale lilikuwa na maana ya kila akitaka kukamatwa anateleza", amesema SACP Mambosasa.

Akizungumzia hali ya usalama ndani ya Jiji hilo, Mambosasa amesema kuwa bado wanaendelea kuwasaka wale wote, wanaotaka kuleta taswira tofauti ili kabla hawajatimiza lengo lao wawafikie na Jiji liendelee kuwa salama.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post